Home Habari za michezo MO DEWJI:- NIMEPOTEZA BILIONI 51 TOKA NIINUNUE SIMBA…

MO DEWJI:- NIMEPOTEZA BILIONI 51 TOKA NIINUNUE SIMBA…

Habari za Simba SC

Mahojiano ya Mohamed Dewji na The Ahmed Mahmood Show amesema kuwa kitu ghali zaidi alichonunua kwenye maisha yake ni klabu ya mpira ambapo ameweka wazi kuwa aliinunua klabu ya Simba miaka mitano iliyopita.

“Nadhani kitu ghali zaidi nilichowahi kununua ni klabu ya mpira inaitwa Simba inamashabiki milioni 35, niliinunua hii klabu miaka mitano iliyopita, nimepoteza takribani Dola za marekani milioni 4 (Tsh bilioni 10.2) kwa mwaka mmoja na kwa miaka yote mitano nimepoteza Dola za Marekani milioni 20 (Tsh bilioni 51).

“Nimeifanya Simba kuwa kwenye orodha ya vilabu 10 Bora Afrika inaleta furaha kwa watu na Afrika pia ni furaha kwangu,” Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji akizungumza kwenye Podcast ya Ahmed Mahmood.

Itafahamika kuwa mchakato wa Mo Dewji kununua hisa za Simba bado haujafikia mwisho kwani bado upande wa Serikali kupitia FCC na RITA bado hawajatoa majibu ya kina kuhusu mustakabali wa mchakato huo.

Mo Dewji alishinda zabuni ya kununua hisa za Simba mwaka 2017 ambapo kwenye tenda hilo alipaswa kulipa Tsh Bilioni 20 kama gharama ya hisa asilimia 49.

Inaelezwa kuwa katika mchakato huo, Mo Dewji alishindanishwa na Said Salim Bakhresa ambaye kwake alijikuta anakwaa kisiki cha kanuni za FIFA zinazokataza mtu/kampuni kuwa na umiliki wa timu zaidi ya moja kwenye daraja moja la ligi.

SOMA NA HII  DAKIKA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA YANGA LEO...MGUNDA AITA MASHAHIDI TAIFA...