Home Habari za michezo PACOME:- MECHI NA AL AHLY DUA ZENU ZINAHITAJIKA SANA….NI WAGUMU MNOO..

PACOME:- MECHI NA AL AHLY DUA ZENU ZINAHITAJIKA SANA….NI WAGUMU MNOO..

Habari za Yanga leo

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua amesema wanahitaji sana mchezo na nafasi ya kwanza katika kundi lao la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kutafuta pointi tatu dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Yanga wako kundi D wakiwa na alama nane na Al Ahly anaongoza kundi akiwa na pointi tisa na timu hizo tayari zite zimetinga robo fainali, Ijumaa hii zinakutana katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo ya Kimataifa.

Kiungo huyo amesema wako Misri wakiwa wanahitaji sana mchezo pamoja na nafasi ya kwanza, kufikia hayo wanatakiwa kujituma kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kusaka ushindi.

Amesema anaimani ya kufanya vizuri katika mchezo huo kwa sababu wanafahamu ubora na madhaifu ya wapinzani wao licha ya kuwa mechi ya ushindani, Wananchi waongeze dua kwa sababu ni watu wenye upendo sana.

“Tunatambua utakuwa mechi ngumu kwa sababu wapo nyumbani, lakini tumejiandaa vizuri na tunaitaka hii mechi kutafuta ushindi ambao utatufikisha kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa kundi letu,” amesema Pacome.

Ametoa siri ya kutokuwa na kiwango bora kwenye mechi ya CR Belouizdad waliocheza hapa nyumbani kwa sababu aliumia siku moja kabla ya mcheso huo ambapo alikuwa katika wakati mgumu sana.

“Ilikuwa siku ngumu sana nakumbuka wachezaji wenzangu wote walikuwa tayari kwa mchezo, ilivyofika asubuhi niliufuata viongozi na kocha nikamwambia sidhani kama ni sahihi kwanfu kukaa , nineona mashabiki na wachezaji wenzangu namna walivyojiandaa.

Ilikuwa siku yangu iweje nisiwepo kufanya jambo kwa ajili yao, najivunia kuingia kwenye historia hii kubwa ya klabu kama Yanga kuwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu kutinga hatua ya makundi baada ya miaka 25 pamoja na kuingia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza,” amesema Pacome.

SOMA NA HII  JE' KMC ATAENDELEA KUWA KIBONDE WA YANGA, KAMPENI INAANZA HIVI LEO LIGI KUU