Home Habari za michezo BAADA YA KUBANIWA NA KAGERA JUZI….GAMONDI KUJA NA GIA HII LEO MBELE...

BAADA YA KUBANIWA NA KAGERA JUZI….GAMONDI KUJA NA GIA HII LEO MBELE YA DODOMA…

Habari za Yanga leo

MMABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wanashuka dimbani leo saa 1:00 usiku kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji FC, mchezo , utakaochezwa Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam.

Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu mchezo uliopita wa ugenini na Kagera Sugar, Kaitaba Kagera, ambapo leo amedhamilia kuendeleza ubabe wao katika dimba la Azam Complex ambapo mara ya mwisho waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 na Hausing FC, Kombe la FA

Wakati Yanga akipigia hesabu alama tatu za mchezo nao Dodoma Jiji FC inayonolewa na Kocha Francis Baraza amedhamilia kutafuta alama muhimu mbele ya vigogo hao kwa kuwasoma na kuona ubora na mapungufu ya wapinzania hao.

Yanga inayotumia viungo wake washambuliaji kuweza kupata mabao, huku Pacome Zouzoua akiwa kinara wao wa kufaynga ambaye Dodoma Jiji FC kuweka ulinzi mkubwa.

Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema baada ya suluhu na Kagera Sugar wamesahihisha makosa yao na kujiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Amesema mechi haitakuwa rahisi kulingana na kila timu kujiandaa vizuri lakini wachezaji wake tayari kwa ajili kutafuta alama muhimu ili kujiweka katika mazuri ya kufukia malengo yao ya kutetea ubingwa.

β€œSasa tumerejea baada ya kutoka Kagera katika mcheso mgumu, tumefanyia kazi mapungufu, ikiwemo kutumia nafasi zinazopatikana, tumejipanga kwa ajili vizuri kukabiliana na wapinzani wetu, Dodoma Jiji FC ni wazuri na tutacheza kwa heshima kubwa,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa anaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi chake kulingana na wachezaji ambao wako katika kikosi cha timu hiyo, akiendelea kumkosa kupa wao, Djigui Diarra ambaye alikuwa na timu yake ya Mali iliyoondolewa katika michuano ya AFCON.

Kocha wa Dodoma Jiji FC, Baraza amefanikiwa kuwaona Yanga katika mechi iliyopita na Kagera Sugar, kuona ubora na madhaifu yao na tayari amemaliza kazi yake na jukumu kubwa amewaachia wachezaji wake.

Amesema ameona ubora wa Yanga ikiwemo uimara wa safu yake ya kiungo mshambuliaji huku na kumtumia mara kadhaa Pacome kushambuliaji, wamefanyia kazi kila nafasi na wanashuka dimbani kwa ajili ya kuonyesha mchezo mzuri.

β€œTuna waheshimu Yanga, timu nzuri ina wachezajI lakini tumejipanga vizuri kwa ajili ya kuleta ushindani mkubwa kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama muhimu mbele ya wenyeji wetu hao,” amesema Baraza.

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA...NAHODHA YANGA AFUNGUKA SIRI HII YA KUWACHAPA RIVERS