Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUPEWA OFA YA KIPORO NA TFF….BENCHIKHA KACHEEEKAA KISHA AKASEMA...

BAADA YA SIMBA KUPEWA OFA YA KIPORO NA TFF….BENCHIKHA KACHEEEKAA KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Simba leo

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha mjanja sana. Kocha huyo baada ya kugundua timu hiyo haitashuka tena uwanjani  kuvaana na Mtibwa Sugar, fasta ameamua kuja na mbinu mpya ili kuhakikisha mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast inakuwa nyepesi ugenini kabla ya kuialika Jwaneng Galaxy.

Simba itavaana na vinara wa Kundi B iliyotangulia robo fainali Asec, Ijumaa hii mjini Abidjan, kabla ya kurudi nyumbani mapema mwezi ujao kumalizana na Jwaneng kutoka Botswana na iwapo itapata matokeo mazuri kwenye mechi hizo mbili itafuzu kwa mara nyingine hatuia ya robo fainali na kuzidi kuboresha rekodi zao ndani ya CAF.

Katika kuhakikisha kila kitu kinakuwa freshi, Benchikha amefichua furaha aliyo nayo kwa kuahirishwa kwa mchezo wa Ligi Kuu uliokuwa upigwe kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakiwa wenyeji akiupongeza uongozi wa Simba na Bodi ya Ligi, huku akisisitiza kazi aliyonayo kwa sasa ni kuimarisha eneo la ushambuliaji linalotumiwa na kina Michael Freddy, Pa Omar Jobe na wenzao ili apate mabao, lakini akiwabana pia viungo wakabaji wa timu hiyo.

Eneo la kiungo lina mafundi kama Babacar Sarr, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma, kocha akisema kama maeneo hayo mawili yatazingatia mbinu atakazowapa basi ana matarajio makubwa ya kufanya vizuri zaidi.

Freddy, Pa Jobe na Sarr ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Sinmba katika dirisha dogo lililofungwa mwezi uliopita wakiwamo viungo washambuliaji wazawa, Edwin Balua, Ladack Chasambi na Saleh Karabaka ambao bado wanajitafuta mbele ya mastaa wengine waliowakuwa kikosini kwa sasa.

Benchikha alisema kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni hatua nzuri kwao kwao, timu ilikuwa imecheza mechi nyingi ndani ya muda mfupi na kuwachosha wachezaji, lakini sasa anapata muda wa kujiandaa kwa mchezo huo wa kimataifa wa Kundi B akiamini akirekebisha mambo kazi itakuwa rahisi kwao.

Benchikha alisema kuna maeneo mawili anaenda kuyafanyika kazi na kuyapa mbinu mpya kabla ya kusafiri kwenda Ivory Coast kwa lengo la kutotaka kupoteza mbele ya wapinzani wao hao waliotoka nao sare nyumbani.

“Asec ni timu ngumu na mechi hiyo sio rahisi kabisa kwa upande wetu, licha ya kuwa walishacheza mchezo wa kwanza na wachezaji wanafahamiana ila bado kazi ipo,” alisema Benchikha na kuongeza.

“Kwenye maandalizi haya nitazingatia zaidi eneo la ushambuliajia ili kuwafanya wachezaji wa eneo hilo wawe bora zaidi hasa katika kutumia nafasi na kufunga, lakini pia eneo la kati hawatakiwi kuruhusu bao la mapema na kuhahakikisha wapinzani hawapati upenyo wowote.”

Katika mechi mfululizo ilizocheza Simba tangu kurejea tena kwa Ligi Kuu, timu hiyo imeonekana kutokuwa na moto na licha ya kupata ushindi au kupata pointi mbele ya wapinzani, lakini jasho limewatoka kwa kubanwa na wapinzani wao kuanzia mechi dhidi ya Mashujaa, Azam FC, Gaita Gold na hata hivi majuzi ilipoumana na JKT Tanzania.

Licha ya mechi hizo zote kuvuna jumla ya pointi 10 na kuifanya ipande hadi nafasi ya pili ikifikisha pointi 36 baada ya mechi 15, ikiwa nyuma ya Yanga yenye alama 40, kocha Benchikha alisema bado hafurahishwi na namna timu inavyopoteza nafasi za mabao na pia kuelemewa na wapinzani, japo anakiiri kucheza mfululizo ni tatizo.

Benchikha alisema anaamini wachezaji wakizingatia atakachowaelekeza, huenda furaha ya mashabiki wa Simba ikawa maradufu, kwani timu hiyo ina kikosi imara chenye wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, ila hawajawa watulivu tu.

Mechi dhidi ya Asec, ndio inayoonekana ngumu kwa Simba, kwani haina rekodi ya kushinda ikiwa ugenini dhidi ya wapinzani wao hao wanaoongoza kundi wakiwa na pointi 10 baada ya mechi nne, kuliko mchezo wa mwisho mbele ya Jwaneng ambayo imeonekana sio tishio kwenye kundi hilo hadi sasa.

Hata hivyo, Simba inapaswa kuwa makini kwani misimu miwili iliyopita iliwatoa nishai Kwa Mkapa kwa kuwang’oa rauindi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa kuwafunga mabao 3-1 na kufuzu kwa faida ya bao la ugenini kutokana na ushindi wa 2-0 iliyopata Simba ugenini na kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao 3-3.

Katika mechi ya kwanza baina ya Simba na Asec iliyopigwa Dar es Salaam, Saido Ntibazonkiza aliwafungia Wekundu bao la penalti, huku wageni wakipata kupitia kwa Serge Pokou aliyewasawazishia kipindi cha pili, ilhali Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi tano ikifuatiwa na Jwaneng yenye nne wakati Wydad CA ikiburuza mkia ikiwa na alama tatu.

SOMA NA HII  DABI YA KARIAKOO NGUMU KUMEZA,MANARA APATA KIGUGUMIZI