Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA KMC …GAMONDI APANIA ‘MKAZO’ KWA MABEKI YANGA….

KUELEKEA MECHI NA KMC …GAMONDI APANIA ‘MKAZO’ KWA MABEKI YANGA….

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameonekana kushtushwa na kasi ya Simba katika mechi za hivi karibuni na ameanza kufanyia kazi safu yake ya ulinzi ambayo imeanza kuruhusu nyavu zao kutikiswa.

Kuelekea mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu amesema inabidi afanye kazi ya ziada katika safu yake ya ulinzi, kwa kuwa timu inayomkimbiza nayo kuwania ubingwa ambayo Simba kuonekana na kiwango cha juu kwa mechi zake baada ya mapumziko ya mwezi mmoja na usajili mpya uliofanywa na Wekundu hao wa Msimbazi.

Kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es Salaam baada ya kumalizana na Tanzania Prisons kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, uwanja wa Sokoine Mbeya, hiyo ikiwa ni mechi ya pili kuruhusu bao.

Yanga waliruhusu bao katika mchezo dhidi ya Mashujaa FC kwa ushindi wa bao 2-1 wakiwa uwanja wa nyumbani, Azam Complex na hivi karibuni na Tanzania Prisons kwa kuibuka ushindi kama hu na kuruhusu moja ugenini.

Kocha Gamondi amesema licha ya kuvuna alama tatu katika michezo yao lakini bado suala la kuruhusu bao katika michezo miwili anatakiwa kulifanyia kazi mapema kwenye safu yake ya ulinzi.

Amesema licha ya kupata ushindi lakini wamekuwa wakiruhusu nyavu zao kutikiswa jambo ambalo anaamini hapo baadae litakuja kuathiri kwani wanaweza kupoteza au kupata sare kwenye moja ya mechi, ikawa ni hatari katika mbio zao za ubingwa kwani Simba inaonekana kuwa ya moto hivi sasa tofauti na ile aliyokuwa akiiona awali.

β€œLigi imekuwa na ushindani mkubwa, timu zimefanya maboresho makubwa, tunatakiwa kujiandaa vizuri katika michezo yetu ijayo kuhakikisha tunafanikiwa kuvuna alama tatu lakini tusiruhusu nyavu zetu kutikiswa.

Inapotokea mpinzani anaanza kupata bao la mapema kabla yetu na wengi wao hupenda kupoteza muda itakuwa ngumu, tunatakiwa kulifanyia kazi jambo hilo mapema ikiwemo umakini wa safu ya ulinzi,” amesema Kocha huyo.

Ameongeza kuwa anahitaji kufanya mabadiliko hayo mapema zaidi kwa kusahihisha kuanzia safu ya ulinzi akiamini nafasi ya washambuliaji haina tatizo kubwa kwa sababu viungo na mawinga hufanya jukumu hilo la kufunga.

Kocha Gamondi amesema mechi ijayo wanarudi na KMC FC mzunguko wa pili, mechi ya kwanza aliwafunga bao 5-0 lakini anaimani hawatakuja watabadilika na kuja kivingine hali ambayo analazimika kuandaa kikosi chake kwa ajili ya ushindi ma kutoruhusu bao.

Yanga itawakaribisha KMC FC ukiwa mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakaochezwa Februari 17, mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MO DEWJI KUKWAMISHWA KUWEKEZA SIMBA...USHAURI ALIOPEWA HUU HAPA..