Home Habari za michezo GAMONDI ALIA KUKAMIWA NA TZ PRISON….MWANYETO AJILIPUA NA KADI YA METACHA…

GAMONDI ALIA KUKAMIWA NA TZ PRISON….MWANYETO AJILIPUA NA KADI YA METACHA…

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amekiri kukutana na presha kubwa kutoka kwa wapinzani wao Tanzania Prisons, kikubwa anafurahi amepata alama tatu muhimu katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema licha ya kucheza vizuri , bado kuna kazi ya kufanya kwenye safu yake ya ulinzi kwa kufanyia kazi kwa sababu katika michezo miwili wameruhusu bao mbili ikiwemo mchezo wa juzi.

Yanga juzi iwalikuwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo huo uliochezwa uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya, Wananchi wakiendeleza ubabe wao wa kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-1.

Ni mchezo wa pili kwa Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo kuruhusu bao jambo ambalo Gamondi ahitaji kuona mechi ijayo inajirudia na kufanyia kazi katika uwanja qa mazoezi

Amesema anafuraha kubwa ya kupata alama tatu muhimu kulingana na wapinzani wao kuwaontesha ushindani mkubwa, hasa kipindi cha pili kuwapa nafasi ya kucheza.

“Pointi tatu ni muhimu sasa licha ya kucheza kwa presha kubwa, kipindi cha kwanza tulicheza vizuri tukatengeneza nafasi na kuzitumia mbili licha ya wapinzani kupata bao moja. Kipindi cha pili hatukucheza vizuri,” amesema Gamondi.

Ameeleza kuwa anarudi uwanja wa mazoezi kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza kujiandaa na mechi ijayo kuhakikisha wanafanikiwa kuvuna alama tatu na kutoruhusu nyavu zao kutikiswa.

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kadi nyukundu aliopewa kipa wao, Metacha Mnata iliwaathiri na kubadilisha mfumo na kucheza mabeki watatu kabla ya wapinzani wao nao kupewa kadi nyukundu na wote kuwa idadi sawa ya wachezaji uwanjani.

“Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri sana kwao na kutengeneza nafasi nne na kufanikiwa kupata bao 2, kipindi cha pili walifanya makosa na kuruhusu kufungwa bao moja. Kwa sasa wana changamoto ya majeraha kwa mabeki hali hiyo kocha amekuwa akifanya mabadiliko katika nafasi hiyo,” amesema Mwamnyeto.

SOMA NA HII  WANAIJERIA WAIPA MBINU SIMBA KUIMALIZA YANGA KWA MKAPA