Home Habari za michezo MASTAA HAWA WA YANGA ‘WAMTIA TUMBO JOTO’ KOCHA WA CR BELOUIZDAD…

MASTAA HAWA WA YANGA ‘WAMTIA TUMBO JOTO’ KOCHA WA CR BELOUIZDAD…

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa CR Belouizdad, Marcos César Dias de Castro maarufu kama Marcos Paquetá (65) amesema kuwa anawaheshimu Yanga SC kwani wanayo timu nzuri na kocha mzuri hivyo mchezo wao wa kesho utakuwa mzuri pia.

Mbrazil huyo amesema hayo wakati wa mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi, Faebruari 24, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 jioni.

“Nina furaha kwamba hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, ninaamini mchezo utakuwa mzuri na mashabiki watafurahia. Ninajua Tanzania kuna timu nzuri na Yanga wana timu nzuri, wanapenda kucheza soka kama sisi ninaamini kila mmoja atafurahia mchezo huu.

“Tangu mwanzo niliona kundi letu ni gumu, sio kundi ambalo mtu anaweza kusema anashinda kabla mechi hazijamalizika. Tumejaribu mechi baada ya mechi lakini mechi ya kesho ni muhimu kwetu.

“Tulishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga lakini kwa sasa ni hali tofauti na mazingira tofauti. Tuko tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, malengo yetu ni kufuzu na si kingine,” amesema amesema Marcos Paquetá.

MASTAA HAWA WA YANGA WAMTIA TUMBO JOTO.

Unaambiwa aarifa za kiufundi za baadhi ya wachezaji hatari wa klabu wa Yanga SC tayari zimekabidhiwa kwa kocha mkuu wa CR Belouizdad, Marques Paquetta kwaajili ya kutafuta dawa ya kuwazuia wasiigharimu timu yao katika mchezo ujao wa CAF Champions League Jumamosi hii pale Benjamin Mkapa Stadium.

Majina yaliyomfikia kocha Marques Paqueta ni zaidi ya matatu lakini yaliyowekewa msisitizo ni majina ya beki Mtanzania Ibrahim Bacca, kiungo mahiri Mganda, Khalid Aucho, pamoja na Pacome Zouzoua.

Yanga na Belouizdad watakuwa dimbani kesho kukipiga katika mchezo wa raundi ya tano ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  ORODHA YA WANAOAWANIA TUZO 2020/21 LIGI KUU BARA V LIGI KUU YA WANAWAKE TANZANIA