Home Uncategorized AZAM FC BADO WANAUHITAJI UBINGWA

AZAM FC BADO WANAUHITAJI UBINGWA

 


KIUNGO wa Klabu ya Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amefunguka kuwa changamoto ya kupata matokeo mabaya kwenye michezo yao iliyopita ya Ligi Kuu Bara haijawaondoa kwenye plani zao, kwani bado wanaamini wana nafasi kubwa ya kupambania ubingwa msimu huu.

  Azam ilianza kwa kasi msimu huu kwa kushinda michezo saba mfululizo,ilipunguzwa na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa kufungwa bao 1-0.


Jana Novemba 30 ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United, Uwanja wa Karume na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 26 ikiwa nafasi ya pili na ile ya kwanza ipo mikononi mwa Yanga yenye pointi 31.

 

Sure Boy amesema matokeo hayo mabaya ni sehemu ya mpira na wanachokifanya hivi sasa ni kurekebisha makosa yao na kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanashinda michezo ijayo.

 

“Kama timu ambayo ina malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu ni wazi tulikuwa kwenye wakati mgumu sana kutokana na matokeo mabaya kwenye michezo yetu iliyopita.

 

“Lakini kwenye mchezo wa soka kuna wakati mnaweza kukutana na matokeo ambayo hamkuyatarajia na hatupaswi kukata tamaa, bali kurekebisha makosa yetu na kujipanga kwa ajili ya michezo yetu ijayo.


“Ukiangalia nafasi tuliyopo kwenye msimamo na michezo tuliyocheza mpaka sasa utagundua kuwa bado tuna nafasi ya kupambania ubingwa msimu huu,” amesema Sure Boy.

 

Sure Boy msimu huu amehusika kwenye mabao mawili ya Azam akifunga bao moja na kuasisti bao moja.

 

SOMA NA HII  RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO OKTOBA 31