Home Uncategorized KOCHA YANGA ATAJWA KUIBUKIA NDANI YA AZAM FC

KOCHA YANGA ATAJWA KUIBUKIA NDANI YA AZAM FC


 IMERIPOTIWA kuwa aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Yanga, George Lwandamina yupo kwenye hesabu za Klabu ya Azam FC kubeba mikoba ya Aristica Cioaba.

Cioaba alifutwa kazi Novemba 26 siku moja baada ya kupoteza mchezo wake mbele ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Deus Kaseke.

Habari kutoka Zambia zimeeleza kuwa Lwandamina yupo kwenye mazungumzo na Azam ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuukosa kwa muda mrefu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea hivyo wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.


“Tumetoka kumaliza mchezo wetu dhidi ya Biashara United jana, kwa sasa timu ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, (Vivier Bahati) hivyo bado hakujawa na taarifa kutoka kwa uongozi kuhusu jina lake.


“Haina haja ya kuwa na haraka kwani bado tuna muda na tunapaswa tufanye mambo kwa utulivu, mashabiki wasiwe na mashaka mchakato wa kumpata kocha mpya unaendelea,” amesema.


Mchezo wa jana, Novemba 30 Azam iligawana pointi mojamoja na Biashara United na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 26 baada ya kucheza mechi 13.

SOMA NA HII  Amunike kujaribu wengine leo