Home Habari za michezo PAWASA:- SARE YA JANA SIMBA WALIKOSEA KWA KIBU TU….BOCCO NI BORA KULIKO...

PAWASA:- SARE YA JANA SIMBA WALIKOSEA KWA KIBU TU….BOCCO NI BORA KULIKO FREDY…

Habari za Simba leo

Nyota wa zamani wa klabu ya Simba Boniface Pawasa baada ya Simba kutoshana nguvu ya bila kufungana na klabu ya Asec Mimosas kwenye dimba la Stade Felix Houphouet Aboigny amesema kuwa hakuona umuhimu wa Kibu Dennis kuanzia Benchi.

Kwa upande mwingine Pawasa ameweka wazi kuwa mshambuliaji mpya wa klabu ya Simba Freddy Koublan anazidiwa kwa kiasi kikubwa uwezo na nahodha wa klabu hiyo John Bocco.

Beki wa zamani wa Simba SC Boniface Pawasa ametoa maoni yake kuhusiana na sare ya 0-0 ya Simba SC dhidi ya Asec Mimosa ugenini.

“Kwa mimi sikubaliani na Mwalimu kwenye muda wa mabadiliko tulikuwa tunamuhitaji Kibu toka kipindi cha pili kilipokuwa kinaanza, siwezi pia kuwa muumini wa Mwalimu kwa mshambuliaji (Fredy) aliyeingia.

Siku ya kwanza nilipomuona katika mechi mbili (Fredy) labda niseme bado anahitaji muda lakini binafsi sielewi kwa nini Simba walimuacha Baleke kati ya Fredy na Bocco mimi naondoka na Bocco.”

Baada ya sare hiyo, Simba sasa imefikisha alama 6 ikiwa nyuma ya Asec Mimosas yenye alama 11 na itahitaji ushindi dhidi ya Jwaneng Galaxy mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...MO DEWJI AWATANGAZAA 'BONASI' YA KIBABE WACHEZAJI SIMBA...