Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA NIGER…TAIFA STARS MAMBO NI ‘NGINJA NGINJA’….

KUELEKEA MECHI NA NIGER…TAIFA STARS MAMBO NI ‘NGINJA NGINJA’….

Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania, Taifa Stars Adel Amrouche ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger.

Stars itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi huo na imewasili salama Morocco kwa ajili ya mchezo huo kwa ndege iliyotolewa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu.

Maandalizi yameanza ambapo mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Grand Marrakech Annex 1, Morroco kuelekea mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger utakaochezwa kwenye mji wa Marrakech Jumamosi Novemba 18, 2023.

Kocha huyo amesema: “Tunafurahi kuwa hapa na kufika salama na maandalizi ya mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Mchezo mgumu na mpira unahitaji matokeo ya furaha hicho ndicho ambacho ninakijua hivyo nina amini itakuwa hivyo mashabiki watafurahi,”.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA APEWA MIAKA MIWILI RWANDA