Habari za Michezo
Habari za michezo

IHEFU, MBEYA KWANZA NA SINGIDA FG KUBADILISHWA MAJINA…MCHONGO WOTE UKO HIVI…

admin March 1, 2024 11:43 am

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zinasema kuwa klabu ya Ihefu yenye maskani yake mkoani Singinda inampango wa kubadilisha jina na kuwa Singida Leopards FC kuanzia msimu ujao.

Ihefu kwa sasa inatumia uwanja wa CCM Liti na wataanza kuutumia kwenye mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mashujaa ya mkoani kigoma.

Hata hivyo ripoti zinaeleza klabu ya Mbeya kwanza ipo mbioni kununuliwa na kubadilishwa jina kuwa Ihefu na watautumia uwanja wa Ubaruku uliopo Mbarali Jijini Mbeya.

Wakati huo huo Singida Fountain Gate itabadili jina pia na kuwa Fountain Gate Academy na maskani yake yatakuwa mwanza kwenye uwanja wa Fountain Gate uliopo Gwambina mara baada ya uwanja huo kufanyiwa marekebisho.

BAADA YA GUEDE KUANZA KUTUPIA YANGA…AZIZ KI AFICHUA KILICHOKUWA KINAMTIA UGUMU… SIMBA WANAPASWA KUJUA UKWELI HUU KABLA YA MECHI YA KESHO…WAKIZUBAA IMEKULA KWAO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply