Home Habari za michezo ALICHOKISEMA GAMONDI BAADA YA YANGA NA PACOME KUFUNIKWA JANA NA AL AHLY…

ALICHOKISEMA GAMONDI BAADA YA YANGA NA PACOME KUFUNIKWA JANA NA AL AHLY…

Habari za Yanga leo

BAADA ya kupoteza bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly nchini, Misri, Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema sasa mawazo yake ameyaelekeza kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, akizipigia mahesabu pointi 12 za michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mechi hizo za Ligi , Yanga watakuwa ugenini dhidi ya Namungo FC Machi 8, 11, watakuwa nyumbani ikiwakaribisha Ihefu FC, Machi 14 na 17, mwaka huu watacheza na Geita Gold FC na Azam FC.

Kikosi cha Yanga kimemaliza nafasi ya pili katika Kundi D wakiwa na pointi 8, kinarejea nchini leo kikitokea nchini Misri katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya Al Ahly inayongoza wakikusanya alama 12.

Kocha Gamondi amesema mechi ilikuwa ya ushindani mkubwa wachezaji walicheza vizuri lakini haikuwa bahati kwao.

Amesema mchezo mzuri, lakini wamepoteza sasa wanarudi kujiandaa na lufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kujiweka sawa katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo michezo yao minne kabla ya kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa

“Tulipata nafasi tukashindwa kuzitumia kwa sababu ya kutokuwa makini na tunarejea nyumbani kusahihisha makosa yetu kujiandaa na hatua inayofuata lakini kwanza tunaangalia kilichopo mbele yetu michezo ya Ligi Kuu,” amesema Gamondi.

Ameongeza kuwa Al Ahly wametumia nafasi vizuri na mechi hiyo imewapa kitu cha kufanyia kazi katika maandalizi ya michezo ijayo ikiwemo robo fainali licha ya sasa wanaangalia michezo minne ya Ligi.

Naye Meneja wa Yanga, Walter Harrison amesema kikosi kimerejea jana kujiandaa na michezo ya ligi , wachezaji walipambana haikuwa bahati kwao na sasa wanaangalia mechi za ligi.

“Tuna mechi nne za ligi tunahitaji kupata matokeo katika mechi hizo, ligi itakuwa kwenye mapumziko kupisha wiki ya Fifa baada ya hapo tutakuwa na maandalizi yetu ya kujiandaa michezo ya robo fainali,” amesema Walter.

SOMA NA HII  AHMEDA ALLY:- VIONGOZI SIMBA TUNAPASWA KUJITAHMINI KWA HALI YA TIMU ILIVYO...