Habari za Michezo
Habari za michezo

KISA ISHU YA ‘MAJINI NA WACHAWI’….MAYELE NA MORRISON WATUPIANA MANENO …

admin March 2, 2024 7:50 pm

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya FAR Rabat ya Morocco ambaye ni raia wa Ghana, Bernard Morrison na mshambuliaji wa Klabu ya Pyramids FC ya Misri, raia wa Congo DR, Fiston Mayele wameibua jambo mtandaoni.

Hii ni baada ya Morrison ambaye amewahi kuchezea Yanga, kupitia ukurasa wake wa Instagram kuandika;

“Sio kwa sababu niliacha kutumia magongo utanitumia Majini. Nitawapeleka tu Zanzibar na watasahau hata ni Majini. Imagine Ghost smoking shisha utaenjoy wallah.”

Baada ya Morrison kuandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram mshambuliaji wa Pyramids, Fiston Mayele ambaye amewahi kuichezea Yanga pia wakiwa pamoja na Morrison, amekuja kwenye post hiyo na kuandika;

“Come back to Morocco are looking for you there witch.” Kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi “Rudi Morocco wanakutafuta wewe mchawi”

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Mayele aliingiabkwenye mzozo na mashabiki wa Yanga akidai kuwa wamemtupia majini ndiyo maana hafungi mabao siku hizi.

NANI BORA KATI YA PACOME NA CHAMA..?..KOCHA LA CAF LAMPA TUZO HUYU… A-Z 6G ZA SIMBA ZILIVYOWATAPISHA NYONGO JWANENG…..CHAMA AACHA MSHANGAO TAIFA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

One response to “KISA ISHU YA ‘MAJINI NA WACHAWI’….MAYELE NA MORRISON WATUPIANA MANENO …”

  1. Mary Augustino Berege says:

    Pacome ni zaidi ya huyo galasha anayesifiwa wakati hamna kitu.

Leave a Reply