Home Habari za michezo MCHAMBUZI:- CHAMA HANA CHAZIDIA ATAKACHOWAPA SIMBA…WAACHANE NAYE TU…

MCHAMBUZI:- CHAMA HANA CHAZIDIA ATAKACHOWAPA SIMBA…WAACHANE NAYE TU…

Habari za Simba leo

Mchambuzi wa soka Wilson John Oruma amesema umefika wakati wa Simba SC kuachana na kiungo wao mshambuliaji, Clotous Chama kwani hakuna cha ziada atakachowapa.

Oruma amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya Chama kuubeba mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy na kuibuka na ushindi wa 6-0.

Oruma amesema, Chama amekuwa akicheza ana akili za viongozi kwani hufanya vizuri pindi mkataba wake unapokuwa unaelekea ukingoni.

“Chama ana jambo lake ndio maana anafanya hivi alivyofanya, baada ya muda atarudi kwenye desturi yake kama kawaida. Ni wakati sasa viongozi kuchukua maamuzi magumu ya kuachana naye ili walete mchezaji anayeweza kuwavusha zaidi ya hapa,” alisema Oruma.

SOMA NA HII  CHEKI BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA V YANGA