Habari za Simba leo
Habari za michezo

“INONGA WA AFCON SIO HUYU WA SIMBA….ANA UTOTO MWINGI SANA….”

admin March 11, 2024 2:12 pm

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa beki wa timu hiyo, henock Inonga ana utoto mwingi jambo ambalo limekuwa likiighalimu timu yake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Simba tulikuwa tunavimba beki la AFCON, nilishawahi kuwaambia Inonga akija Simba ana masihara mengi. Inonga wa AFCON sio Inonga wa Simba, ana utoto mwingi.

“Bao la pili tumefungwa sababu yake, Mbangula amemzunguka akajiangusha anajifanya ameumia. Timu inahitaji uiokoe halafu unaleta utoto kama huo? Anatoka anasema ameumia bila kuguswa na mtu yeyote, anaighalimu timu,” amesema Mapovu.

KUELEKEA DROO YA CAF KESHO….GAMONDI AFUNGUKA ‘PLAN’ ZA KUTINGA NUSU FAINAL KIBABE… SHABIKI SIMBA:- KWA MWENDO HUU YANGA BINGWA TENA…MZAMIRU NO 10 TANGU LINI…?

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply