Home Habari za michezo DROO YA CAF LEO…..GAMONDI ANATAKA YEYOTE YULE ANAYEJIAMINI….MAMELOD MHHHH….

DROO YA CAF LEO…..GAMONDI ANATAKA YEYOTE YULE ANAYEJIAMINI….MAMELOD MHHHH….

Habari za Yanga leo

WAKATI Droo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika inapangwa leo, Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi ameandaa timu yake kukutana na yeyote katika hatua hiyo kuhakikisha wanafanya vizuri.

Aliyasema hayo jana baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu FC na Yanga akiibuka na ushundi wa mabao 5-0 , mchezo huo utakaochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.

Yanga inaweza kukutana na moja ya timu tatu akiwemo Asec Mimosas ya Ivory Coast, Pretro de Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Gamondi amesema anatambua timu zote zilizoingia hatua ya robo zote ni nzuri na wapo tayari kukutana na yoyote na hawana presha kwa sababu kutumia michezo ya ligi kuu kwa ajili ya kuandaa timu yake ya robo fainali.

Kuhusu mchezo wa jana na Ihefu FC, Kocha huyo amesema haikuwa rahisi , ameridhika na jinsi wachezaji walivyofanyia kazi mpango wao wa mchezo huo na ameeleza sababu za mabadiliko ya mbinu na wachezaji kipindi cha pili.

Gamondi amesema waliwaheshimu Ihegu FC, walicheza vizuri sana na walijitahidi kumiliki mpira, walitengeneza nafasi nyingi na kuzitumia baadhi na kufanikiwa kushinda mabao 5-0.

Amesema kipindi cha kwanza Ihefu ilicheza na watu wengi kwenye eneo lake la ulinzi lakini walikuwa na mbinu nzuri na walifanyia kazi hilo kwa kulitafutia ufumbuzi.

“Kipindi cha pili Ihefu FC walikuja kwa nguvu ili kutaka kupata mabao , tukafanya mabadiliko ya kimbinu kwa kumuingiza Guede (Joseph) na Okrah (Augustine) kwa lengo la kutumia kazi yake (Okrah) keenye mashambulizi ya kushukiza ‘Counter attack’s’ na ilitulipa.

Mara zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangi tucheze kama tulivyofanya mazoez na tumeonyesh kile ambacho tulikuwa ttukikifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi,” amesema Gamondi.

Kinara wa mabao wa Yanga, Stephane Aziz Ki amesema mechi ilikuwa nzuri na wanafurahi kupata ushundi wa mabao 5-0, licha ya kukutana na timu iliyowafunga mzunguko wa kwanza hawakuwa na presha kwa sababu Yanga ni timu ngumu, nzuri na wachezaji wapambanaji na walikuwa tayari kutafuta point tatu dhidi ya Ihefu FC.

“Hakuna siri yoyote juu ya uwezo wangu wa kufunga kwa msimu huu zaidi kuwa na timu imara , benchi la ufundi imara zaidi kucheza kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji wangu kuwasiliana vizuri na kujipanga katika nafasi.

Kuhusu droo ya CAF na timu tunayokuna nayo hatua ya robo fainal, hatuna presha na yoyote tupo tayari na tutakayepangwa naye kwa sababu tuna timu imara hali ambayo hatuna presha ambayo wadau wanafikiria,” amesema Aziz Ki.

Naye Kocha wa IhefuFC, Mecky Maxime amesema kilichotokea hakihitaji maelekezo marefu zaidi ya kusema Yanga walistahili kushinda.

Amesema maelezo yasiwe marefu walistahili kushunda, mechi ilikuwa wazi walipata nafasi wakashindwa kuzitumia na Yanga wakatumia uwazi huo na kuadhibiwa.

“Tumeadhibiwa na timu bora leo (jana) sina neno lolote la kusema zaidi zaidi ya kuwapongeza Yanga kwa kucheza vizuri na kuzitumia nafasi walizozipata vema,” amesema Mecky.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI HUYU AWAOGOPA WANANCHI..."HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUCHEZA NA YANGA