Kocha wa Zamani wa Yanga SC, Cedric Kaze kuelekea mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns amewapa ushindi Mamelodi bila uoga
“Kuanzia msimu huu umeanza Yanga haijawahi kubadili aina yake ya uchezaji.. hii mechi itakuwa nyepesi kwa Mamelodi japo ushindani utakuwepo kwasababu timu zote mbili zinaweza kumiliki mpira na kupiga pasi nyingi..” amesema Kaze
MCHAMBUZI AWAUA MASTAA YANGA..
Mchambuzi wa soka Bongo, Nasri Khalfan amesema kwenye kikosi cha Mamelodi Sandowns wapo wachezaji ambao wanaanzia benchi lakini wakija Yanga SC wanaanza kikosi cha kwanza.
Hiyo imekuja baada ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe kusema wachezaji saba wa Yanga wanaweza kuanza kikosi cha kwanza pale Mamelodi.
“Sikubaliani na kauli kuwa kuna wachezaji 7 wa Yanga wanaanza moja kwa moja kikosi cha Yanga, Kiuhalisia kuna Wachezaji wanakaa Benchi Mamelodi Sundowns lakini wakija Kikosi cha Yanga ndio wanaanza moja kwa moja vizuri tuβ @nasrikhalfan_ kuhusu kauli ya Ali Kamwe.