Home Habari za michezo BAADA YA ‘KUWAPASUA’ NAMUNGO JANA….GAMONDI AJIPA UBINGWA WA LIGI KUU…

BAADA YA ‘KUWAPASUA’ NAMUNGO JANA….GAMONDI AJIPA UBINGWA WA LIGI KUU…

Habari za Yanga SC

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Namungo FC, Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema ameridhishwa na kiwango cha nyota wake, huku sasa akiwa na matumaini ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

Yanga waliibuka na ushindi huo juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Kocha Gamondi, amesema ameridhishwa kiwango cha wachezaji na kuwataka wapambane zaidi kwani kwa hali waliyofikia, matumaini ya kupata ubingwa ni mkubwa.

Amesema alizungumza na wachezaji wake kabla ya mchezo na kuwaambia kama wanahitaji ushindi wanapaswa kucheza kikubwa na kwa malengo jambo ambalo walifanikiwa.

“Tunachohitaji ni kushinda kila mchezo kuweza kutetea ubingwa, mapema kuzungumzia hilo lakini ushindi ndio silaha pekee, itatupa tunachohitaji, kwa sasa tunaenda hatua kwa hatua kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” amesema Gamondi

Ameongeza kuwa katika mchezo huo katika kipindi cha kwanza nyota wake walikosa nafasi lakini baada ya kupumzika walilazimika kuongeza juhudi na kufanikiwa kupata mabao.

Kiungo wa timu hiyo, Mudathir Yahya amesema walihitaji pointi tatu sana, kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu sana, walipambana na kujituma kwa kuvuka alama muhimu kujiimarisha katika nafasi yetu ya kuongeza msimamo.

“Hii mechi tulihitaji pointi tatu , kocha alituambia lazima tupambane na kujituma ili kuvuna alama hizo basi tucheze kikubwa na hili limefanikiwa, suala la bingwa bado ligi inaendelea na bado tunaviporo na kutakiwa kushinda,” amesema Mudathiri.

Yanga inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 46 baada ya kushuka dimbani mara 17, imeshinda michezo 15, imetoka sare na kufungwa mchezo mmoja mmoja wakati ikifunga mabao 42 na kufungwa mabao tisa.

SOMA NA HII  SADIO KANOUTE 'AMBALAGAZA' MZAMIRU SIMBA...JAMBO LAKE LAENDA KAMA ALIVYOTAKA...