Home Habari za michezo FT:- AL AHLY 1-0 YANGA…..PACOME AZIMWA KININJAA NA WAARABU….REKODI YASHINDIKANA….

FT:- AL AHLY 1-0 YANGA…..PACOME AZIMWA KININJAA NA WAARABU….REKODI YASHINDIKANA….

FT:- AL AHLY 1-0 YANGA

Yanga imeshindwa kuvunja rekodi ya Al Ahly iliyodumu tangu mwaka 1982 ya timu za Tanzania kuibuka na ushindi kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

Ahly haijawahi kupoteza mechi yoyote nyumbani mbele ya klabu za Tanzania na imeendelea kusalia kileleni mwa kundi D na pointi 12 huku Yanga akibaki nafasi ya pili na pointi 8 zote zikiwa zimeshafuzu robo fainali

Belouizdad imemaliza nafasi tatu sawa na Yanga baada ya kumchapa Medeama mabao 3-0 leo katika Uwanja wa 5 July 1962, Algeria.

Makosa waliyofanya mabeki wa Yanga dakika ya 46 ya mchezo, yalitosha kuipa Ahly ushindi huo mwembamba kwa bao safi lililofungwa na Hussein El Shehata.

Yanga ambayo ilianza mchezo huo bila kiungo wake, Maxi Mzengeli ambaye hata kwenye benchi hakuwepo, ilionyesha kiwango kizuri lakini kwa dakika zote tisini ilishindwa kutikisa nyavu za mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho aliumia na kutoka na aliingia Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kucheza kwenye nafasi yake na kuwapa nafasi Ahly ya kushambulia kwa kasi lakini dakika tisini zilimalizika kwa ushindi huo mwembamba.

Katika mchezo mwingine, CR Belouazdad ambayo ilichapwa mabao 4-0 na Yanga wiki moja iliyopita, imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Medeama na kumaliza katika nafasi ya tatu ya kundi hilo ikiwa pointi nane sawa na Yanga.

Mabao ya CR yalifungwa na Raouf Benguit, Leonel Wamba na Jallow na kuwafanya Medeama wamalize mkiani na pointi nne.

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO, BEI YA JEZI MPYA ZA YANGA NI HII...UZI WA NYUMBANI WABADILIKA RASMI...