Home Habari za michezo JICHO LA NABI LAANGUKIA KWA MASTAA HAWA 3 WA YANGA….ANAWEZA KUWASAJILI..? JIBU...

JICHO LA NABI LAANGUKIA KWA MASTAA HAWA 3 WA YANGA….ANAWEZA KUWASAJILI..? JIBU HILI HAPA..

Habari za Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye anaendeleza moto katika Ligi Kuu ya Morocco akiwa na FAR Rabat, huku akiendelea kuifuatilia timu hiyo, amesema anafurahi kuona ilivyo ya moto na kuwataja wachezaji watatu wanaibeba timu hiyo, akitahadharisha wapinzani kwamba watapata tabu sana kama wasipoji-panga vyema.

Kule Morocco kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama Botola Pro, Nabi ameiweka FAR juu ya msimamo ikiongoza ligi kwa pointi 49 ikiwa na mchezo mmoja mkononi, ikifuatiwa na Raja Athletic yenye pointi 48 na rekodi zinaonyesha katika mechi 10 zilizopita ameiongoza timu hiyo kushinda mechi nane, kutoka sare mbili.

Pamoja na moto wa timu yake kama alivyoiacha Yanga kwenye Ligi Kuu Bara, Nabi amesema amekuwa akii-fuatilia timu hiyo na kulidokeza Mwanaspoti kuwa anafurahia kuona inavyoendeleza moto kwenye ligi ya ndani na kimataifa.

Nabi alisema Yanga ni familia yake aliyoishi nayo kwa mafanikio kwa miaka miwili na kwamba hatua ya kui-fumua Simba kwa mabao 5-1 katika Kariakoo Derby, alizifurahia zaidi akikumbuka utamu wa ushindi mkubwa kama huo.

Nabi alisema Yanga imeendelea kuwa na matokeo mazuri uwanjani ndani na nje ya nchi kutokana na namna ambavyo kikosi chao kinasukwa kimkakati wa muda mfupi na ule wa muda mrefu.

“Nafurahi sana kusikia Yanga inafanya vizuri, hiyo ni familia yangu, sijaondoka kwa ubaya Yanga ni familia ambayo niliachana nayo kwa muda huku nikiwa na huzuni kubwa moyoni, nafurahi kuona mambo yanaendelea vizuri hapo hata ilipowafunga Simba mabao matano nilikuwa na furaha kubwa najua namna mashabiki wa Yanga na hata viongozi walivyofurahia,” alisema Nabi na kuongeza;

“Naona bado timu ipo imara zaidi, nilikuwa hapo wakati naondoka nilisema kuondoka kwangu hakuwezi ku-wa shida kwa kuwa hata mimi nililetwa hapo na wale walionileta bado wapo na hao hao ndio waliokuwa wanasajili pia wachezaji nikishirikiana nao.

“Mikakati yao ya kusuka timu imara naijua pale Yanga kuna mipango ya muda mfupi na muda mrefu ndio maana unaoana ubora wa timu bado mkubwa, kile kikosi changu kiliendelea kuboreshwa zaidi na zaidi.

ATAJA WATATU

Kocha Nabi aliyetwaa na Yanga mataji sita tofauti, yakiwamo mawili ya Ligi Kuu, ASFC na Ngao ya Jamii amewataja wachezaji wapya kama Pacome Zouzoua, Yao Kouassi na Maxi Nzengeli wamechangia kwa kiasi kikubwa kukipa nguvu kikosi hicho ambacho alikiongoza kuchukua mataji 6 ya ndani na kuifikisha Yanga Fainali ya Shirikisho Afrika.

“Naona kuna wachezaji bora wameongezwa Pacome (Zouzoua), yule beki mfupi wa kulia (Yao) na Maxi. Huyu Maxi nilikuwa namfahamu tuliwahi kumpigia hesabu za kumsajili wakati nikiwa hapo tukasema tumuache kwanza akomae zaidi, hawa watatu ni wachezaji bora sana,” alisema Nabi na kuongeza;

“Jambo zuri ni kwamba walikuja kuungana na wenzao bora zaidi ambao waliwakuta kitu bora zaidi kumeku-wa na muendelezo mzuri wa kuwafanya wale ambao waliwakuta na wale waliokuja nyuma yao waendeleze ubora wao.

“Kwenye Ligi ya Mabingwa naona pia wanafanya vizuri hii imekuwa rahisi kutokana na muendelezo wa ub-ora ambao tulianza nao kwenye Kombe la Shirikisho, sehemu kubwa ya timu ilikuwepo tena yenye ubora, ina-pounganika na wale wachache wenye ubora pia utaona namna Yanga ilistahili kufanya vizuri, nawapongeza sana viongozi, makocha, wachezaji na hata mashabiki.”

SOMA NA HII  SHINDA KIBINGWA NA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET, CHEZA SLOTI YA DEUCES WILD POKER.....!