Home Habari za michezo KISA MECHI NA AL AHLY…BENCHIKHA ATAKA KUKIMBILIA ZNZ KUJICHIMBIA …MPANGO WAKE...

KISA MECHI NA AL AHLY…BENCHIKHA ATAKA KUKIMBILIA ZNZ KUJICHIMBIA …MPANGO WAKE HUU HAPA…

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha hataki masihara kuhusu michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akatisha masomo anarejea Tanzania na kutaka kambi ya Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na robo fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Taarifa za uhakika kuwa, Benchikha aliondoka nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya masomo lakini kulingana na kibarua kigumu ambacho Simba wanakutana nacho katika robo fainali kocha huyo amelazimika kurejea haraka.

Mtoa habari huyo alisema kocha amependekeza timu yake ikaweke kambi visiwani Zanzibar kipindi ambacho Ligi Kuu Tanzania Bara itakuwa imesimama kwa ajili ya kupisha kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA).

“Kocha atarejea mapema kuendelea na majukumu yake, katika michuano hii ya kimataifa Benchikha hana masihara tayari tumeshamfahamu mpinzani wetu na ameweka mikakati yake kuelekea mcheso huo.

Moja na mikakati yake kutumia kipindi cha kalenda ya Fifa kwa timu za Taifa mbalimbali kucheza mechi za kirafiki yeye ameomba timu iende kambi Zanzibar kupata utulivu wa kujiandaa na mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Ahly,” alisema Mtoa habari huyo.

Kikosi cha Simba leo kinashuka dimbani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mashujaa FC, uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.

Kuelekea mchezo huo

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola alisema ligi inashika kasi na kwenda mwishoni, Mashujaa FC walianza vibaya lakini wamebadika sana tofauti na walivyoanza msimu.

Alisema wameona ubora , uzuri na mapungufu ya wapinzani wao hao na wamejipanga vizuri kusaka pointi tatu dhidi ya Mashujaa FC, utakuwa mchezo wa ushindani mkubwa.

“Katika michezo mitatu tumeruhusu kila mechi kama benchi la ufundi tumefanyia kazi na malengo yetu makubwa ni kuona tunapata matokeo mazuri na ushindi dhidi ya Mashujaa FC.

Kwa uhalisia unaona ligi ni ngumu na suala la ubingwa bado upo wazi kaa sababu kuna mechi nyingi na aliyekuwa juu yetu anaweza kupoteza hivyo hatujakata tamaa kuhusu ubingwa, kikubwa ni kushinda dhidi ya Mashujaa,” alisema Matola.

Alisema mabadiliko yanatokana na benchi la ufundi kulingana na mchezo ulivyo lakini na mpinzani ambaye wanaenda kukutana naye kwa wachezaji wote wako fiti.

Alisema licha ya kutafuta pointi tatu katika mechi za ligi, wanatumia mchezo huo kujiandaa na mchezo wa robo fainali dhidi ya Al Ahly, timu ambayo wamekuwa wakikutana nao kila msimu.

“Tukumbuke Al Ahly sasa kwetu sio timu ngeni tumekuaa tukikutana nao na mara ya mwisho tulitoka kwa kanuni, kwa sababu tulitoa sare michezo yote miwili ya African Football League (AFL) kama nilivyosema awali sasa ni muda wa kuzichanga vyema katara zetu,” alisema Matola

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU