Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AL AHLY….CHAMA AVUNJA UKIMYA SIMBA….ATAJA MTITI ULIOPO NDANI…

KUELEKEA MECHI NA AL AHLY….CHAMA AVUNJA UKIMYA SIMBA….ATAJA MTITI ULIOPO NDANI…

Habari za Simba leo

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amekiri kuwa mechi yao dhidi ya Al Ahly katika hatua ya robo fainali, itakuwa ngumu, lakini sasa ni muda wao wa kuandikia historia katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inatarajiwa kuanza nyumbani katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Al Ahly ya Misri unaotarajiwa kuchezwa Machi 29, mwaka huu, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Chama amesema itakuwa mechi ngumu kwa kuwa wanafahamu ubora wa Al Ahly, watacheza kwa kuwaheshimu kwa sababu wanahitaji kufanya vizuri kuandika historia kwa mwaka huu.

Amesema malengo yao makubwa ni kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya Al Ahly kupata matokeo nyumbani, benchi la ufundi litafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika michezo iliyopita kwa ajili ya kufanya vizuri na kufikia malengo ya kuvuka robo fainali.

“Malengo yetu ni kuona tunavuka robo fainali kwa misimu minne tunaishia hatua hii, Al Ahly sio wageni kwetu tumekutana nao mara nyingi timu nzuri na bora lakini hatuwaogopi tunawaheshimuna tuko tayari kupambana,” amesema kiungo huyo aliyeenda kwao kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa.

Ameongeza kuwa anaimani benchi la ufundi litafanyia kazi makosa yaliyojitokeza na kujiandaa kwa ajili ya ya mchezo huo, wachezaji wote wanatambua umuhimu wa mechi hiyo na hawana ugeni na Al Ahly kwa kuwa walikutana nao Tanzania na hata Misri.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO...SIMBA WAPENYEZEWA MBINU YA KUICHAPA MTIBWA MANUNGU...CHAMA ATAJWA..