Home Habari za michezo KUTOKA TANGA….ONANA ALIVYOBADILI UPEPO MBAYA SIMBA…ISHU YA MANULA IMEKAA HIVI…

KUTOKA TANGA….ONANA ALIVYOBADILI UPEPO MBAYA SIMBA…ISHU YA MANULA IMEKAA HIVI…

Habari za Simba leo

MSHAMBULIAJI Willy Onana amerejesha furaha Msimbazi baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi dhidi ya Coastal Union wakiichapa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Licha ya Coastal Union kucheza kwa ustadi ndani ya dakika 70, wakienda sare bao moja moja mabadiliko ya benchi la ufundi yalizaa matunda baada ya Willy Onana kukwamisha mpira nyavuni dakika ya 73.

Onana ameingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Said Ntibazonkiza na alitumia dakika tano tu kuwapa furaha wanasimba waliojitokeza kwenye uwanja huo.

Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku eneo la kiungo vita ikiwa kali kwa pande zote mbili lakini Coastal Union walikuwa bora zaidi.

Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 11, likifungwa na Feddy Michael akiunganisha mpira wa kona uliochongwa na Clatous Chama.

Coastal Union ilitumia dakika 14 tu kusawazisha bao kutokana na kona fupi na mpira kukwamishwa kambani na Mwamba wa Kusini, Lucas Kikoti.

Mabao hayo yalidumu hadi kipindi cha Kwanza kilipoisha, huku kipindi cha pili timu zote zikirudi na nguvu kila mmoja akisaka bao la uongozi, kabla ya dakika ya 73 Onana ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeraruhi, amerudisha furaha msimbazi.

Ushindi walioupata Simba umewafanya wafikishe pointi 39 katika michezo 17 ikibaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 44, huku Yanga akiongoza na pointi 46.

AJIBU VS NGOMA
Haikuwa rahisi katika eneo la kiungo la Simba kufanya udambwi udambwi kama walivyozoeleka. Hii ni kutokana na ubora wa kiungo wao wa zamani, Ibrahim Ajibu ambaye alimpa mtihani Kocha Suleiman Matola kufanya mabadiliko kwa kumtoa Babacar na kumwingiza Mzamiru Yassin.

Ajibu mbali na kuichachafya safu ya kiungo pia alikuwa mwiba kwa mabeki wa kati ambao walikuwa ni Keneddy Juma na Che Malone ambao waliruhusu nyavu zao kutikiswa dakika 25 za kipindi cha kwanza.

KADENA, AISHI, AYOUB NANI ALAUMIWE
Kwenye kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons langoni akiwa Aishi Manula lawama nyingi zilitolewa kwa kipa huyo, anafanya makosa, lakini lakini jana Simba ikiwa na Ayoub ilionkana kurudia makosa na kuruhusu nyavu zake kutikiswa.

Simba ambayo ilifanya mabadiliko ya wachezaji watano kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ilimrudisha Mohammed Hussein kuchukua nafasi ya Israel Mwenda, Che Malon alichukua nafasi ya Henock Inonga, huku Kibu Denis akianzia benchi akimpisha Luis Miquissone.

Licha ya mabadiliko hayo, Simba haikuwa bora kwani ilipata bao moja kipindi cha Kwanza hadi hapo benchi la ufundi chini ya Matola lilipofanya mabadiliko yaliyozaa matunda.

SOMA NA HII  MWAKINYO AFANYA HAYA KWENYE ADHABU YA MANARA TFF