Yanga SC imewachukua muda mrefu Sana kupata mlinda mlango mzuri na mwenye ubora mkubwa Sana kama ilivyo Kwa huyu mlinda mlango wao wa Sasa. Wamepita walinda mlango wengi ndani ya kikosi Cha wananchi, Juma Kaseja, Dida, Mustafa, Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya na wengine wengi lakini kati ya hao hakuna aliyemfikia Diarra Kwa ubora ambao unaendana na mahitaji ya kisasa.
Amekuwa imara sana, Kuna nyakati timu inakuwa inaelemewa lakini Kwa ubora wake Bado anaisaidia timu yake kuwa salama nyakati tofauti tofauti, Mfano msimu uliopita kati ya magolikipa waliofanya saves nyingi na za kutosha ni pamoja na huyu mwamba, kuanzia hatua ya robo fainali msimu uliopita hadi anacheza fainali alifanya saves 16 ambazo pengine asingekuwa golikipa mzuri pengine ingewaletea shida wananchi.
Yanga SC msimu katika michuano ya Klabu bingwa barani Afrika, imeruhusu magoli 6, na kufunga magoli 9, lakini kati ya magoli 6 ambayo kama timu imeruhusu yeye Diarra ameruhusu magoli 3 pekee katika 6 ambayo kacheza bado ni takwimu nzuri Sana kwake na Kwa timu pia.
Akiokoa mchomo wa penati kama mtakuwa mnakumbuka, mchezo kati ya Yanga SC v Medeama FC ya Ghana ambao Yanga SC alishinda goli 3-0 Hiyo Siku Diarra aliokoa mkwaju wa penati.
Juzi pia katika michezo yote miwili kati ya Yanga SC v Mamelodi sundowns FC na ule wa kule Afrika Kusini kati ya Mamelodi sundowns FC v Yanga SC, alifanya SAVES nyingi Sana pengine hata hatua ya matuta wasingefika, ubora wake Kwa Sasa ni sawa na dhahabu, amekuwa Bora mno, umri wake unaruhusu miaka 28 ni umri wa kazi kabisa.
Binafsi naamini itawachukua muda mrefu sana Yanga SC kumpata golikipa mwingine mwenye ubora mkubwa kama huyu kama akaondoka.