Home Habari za michezo “MABOSI SIMBA WAMEMSUSIA TIMU AHMED ALLY….WAO WANAKULA BATA DAR”….

“MABOSI SIMBA WAMEMSUSIA TIMU AHMED ALLY….WAO WANAKULA BATA DAR”….

Habari za Simba leo

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba maarufu kwa jina la GB 64 amesema kuwa viongozi wa timu hiyo wamemwachia Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahemd Ally huku wao wakiendelea na mambo yao binafsi.

GB 64 amesema kuwa si Mwenyekiti wa Klabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CEO wa Klabu ambaye kwa sasa yupo karibu na timu badala yake wamemwachia Ahmed afanye kila kitu jambo ambalo linaifanya timu isipate matokeo chanya uwanjani.

“Klabu Bingwa (CAFCL) tulipotolewa tulisema tumetolewa na Al Ahly timu kubwa, sasa hii ya kutolewa na Mashujaa tusemeje? Hali ndiyo ileile tu kwa Simba. Simba ukiiona imeharibu tu kwenye klabu Bingwa ujue inaporomoka kwenye Ligi, mzunguko wa pili Simba inaboronga saba na sasa inazidi kushuka tu, tusipokuwa makini hali itakuwa ngumu.

“FA tulikuwa tunasihia nusu fainali kwa miaka miwili sasa hivi tumeishia robo kwa kutolewa na Mashujaa tena wakiwa nusu. Morali ya wachezaji imeshuka kabisa.

“Viongozi wamemwachia timu Ahmed Ally (Meneja Habari), yeye ndio bodi yeye ndio mwenyekiti, ndo CEO na ndio kila kitu. Mwajiriwa amekuwa kama ndiye mwanachama wa Simba au mwenye timu. Ukiangalia Jukwaani hakuna Try Again (Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi), Mangungu (Mwenyekiti wa Simba) wala Kajula (CEO wa Simba) wote hawapo wamemwachia Ahmed Ally, morali ya timu itatoka wapi.

“Wenzetu (Yanga) kila inapokwenda timu rais yupo, Makamu yupo, CEO yupo na viongozi wote lakini Simba hata wazee hatuwaoni, Simba haieleweki. Kama wameshindwa kuiendesha timu wajitathimini waiachie, hawawezi kukaa pale milele.

“Yanga sasa hivi inafanya vizuri, pale kuna mwamba anaitwa Injinia Hersi, alianza kwa kukosea na kina Sarpong lakini leo ana kikosi tishio Afrika,” amesema GB 64.

Simba kwa sasa inapitia wakati mgumu ikiwa ni miaka mitatu tangu kifo cha Hans Poppe huku hivi karibuni ikiondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuondoshwa pia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania.

SOMA NA HII  BAADA YA KIKAO..AJIB, MKUDE LIMEWAKA..WASEMA YA MOYONI..WAMUIBUA ZAHERA..MWANASPOTI..