Home Habari za michezo MAYELE:- ENG HERSI ALINISAINISHA MKATABA WA HOVYO SANA NIKIWA YANGA….

MAYELE:- ENG HERSI ALINISAINISHA MKATABA WA HOVYO SANA NIKIWA YANGA….

Habari za Yanga leo

Mshambuliaji wa Klabu ya Pyramids, Fiston Mayele amesema kuwa alifanyiwa mambo ya hovyo na uongozi wa Klabu ya Yanga kabla ya kufanya maamuzi ya kuondoka klabuni hapo.

Mayele ambaye mambo yake yamekuwa si maziri sana huko Misri, amesema hayo wakati akihojiwa na Azam TV huku akibainisha kuwa baadhi ya vioengele vilivyokuwa kwenye mkataba wake wa kwanza na Yanga vilikuwa vya kinyonyaji.

“Mkataba wangu na Yanga wa kwanza ulikuwa mgumu, mimi Kiingereza sijui anayenisimamia na yeye hajui akawa anachekacheka tu na viongozi wa Yanga.”

“Nilivyosaini mkataba wa pili nikaja na msimamizi mwingine sikuja na yule wa kuchekacheka, bali Dada Yasimini kabla ya yote akaomba mkataba wa mwanzo alisikitika sana, mambo nyuma yalikuwa magumu mno, dada wa watu anasaidia sana wachezaji, namshukuru sana,” amesema Mayele.

Aidha, mchezaji huyo ambaye hivi karibuni alionekana na viongozi na baadhi ya wachezaji wa Simba walipokuwa Misri, anatajwa kuwa huenda akajiunga na Simba msimu ujao huku yeye akidai kuwa bado ana mkataba na Pyramids lakini atafunguka mengi aliyofanyiwa na Yanga baada ya kumalizika kwa msimu huu.

SOMA NA HII  SAA CHACHE BAADA YA YANGA 'KUMPANGUSA KAZI'...BUMBULI AIBUKA NA UJUMBE HUU...ATAJA ANAPOENDA KUFANYA KAZI...