Home Habari za michezo MBUNGE:-“MNA CHAMA NA PACOME SISI TUNA MAMA SAMIA…AMEZUNGUMZA HAYA BUNGENI

MBUNGE:-“MNA CHAMA NA PACOME SISI TUNA MAMA SAMIA…AMEZUNGUMZA HAYA BUNGENI

Habari za Michezo leo

Mbunge wa Jimbo la Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde amesema Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kutajwa kwa sababu ndiye mmiliki wa maendeleo ya nchi.

Lusinde amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

“Kuna baadhi ya wachambuzi wanachekesha wanasema watu wanamtaja sana Mhe. Samia badala ya kazi zilizofanyika lakini ukikaa kwenye mpira utaona wanamtaja sana Chama wanamtaja Pacome unaemtaja sana si mwenye mpira?

“Mtu mwenye mpira ndiye anayetajwa sana Dkt. Samia anamiliki mpira wa maendeleo kwenye nchi hii ndio maana tunamtaja sana,..tunamtaja sababu vitu anavyotufanyia ndugu zangu hatujaona serikali ikishusha pesa vijijini kama Rais Samia,” amesema Lusinde.

SOMA NA HII  MASHABIKI MAN UTD WAMALIZIA HASIRA ZOTE MAGUIRE...WAMZOMEA MWANZO MWISHO...