Habari za Simba leo
Habari za michezo

HARMONIZE AMCHANA MO DEWJI…ATAJA SABABU YA SIMBA KUFANYA VIBAYA…AMTAJA BARBARA

Marce Ben Komba April 23, 2024 12:31 pm

Supastaa wa Bongo Fleva, msanii Harmonize anasema tatizo la Klabu ya Simba lilianza baada ya aliyekuwa CEO wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez kujiuzulu wadhifa wake na kuondoka.

Harmonize amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa watani zao Yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi Aprili 20, katika Dimba la Mkapa.

“Nazikumbuka nyakati za Simba ya CEO Barbara ndugu zangu watani mnayo nafasi ya kujiuliza, ni swala la kuheshimu mwanamke tuu. Na kumpa heshima siamini kama Barbara hana mapenzi na Simba tena

“Kwa sababu nakumbuka jinsi alivyoipigania team yenu, mtag @moodewji mara nyingi uwezavyo. Kama unaipenda team yako na unaamini tatizo ni usajili tuu ila Simba sio mbovu.”
Unakubaliana na Jeshi?

WANANCHI WAJIPANGA KUPAMBANA NA WANAJESHI…WAINGIA KAMBINI LEO HII HAPA BLACKJACK 2 YA KWENYE MERIDIANBET AMBAYO INATEMA MPUNGA WAKATI WOTE..