Home Habari za michezo ARSENAL DHIDI YA CHELSEA NI DERBY YA MAAMUZI…

ARSENAL DHIDI YA CHELSEA NI DERBY YA MAAMUZI…

Meridianbet

Leo itakwenda kupigwa mechi ya kibabe sana kwenye ligi kuu ya Uingereza ambapo pia ni Derby kati ya klabu zinazotoka katika jiji moja yaani la London Arsenal dhidi ya Chelsea.

Arsenal watakua wenyeji wa mchezo huu utakaopigwa katika dimba la Emirates usiku wa leo ambapo kila timu ikiutazamia mchezo huu kwa jicho pevu, Kwani kila timu inaweza kunufaika kwa kiwango kikubwa na mchezo huu usiku wa leo na ndio sababu tukasema hii ni Derby ya maamuzi.

Mchezo huu ni muhimu kwa vilabu vyote viwili kwani klabu ya Arsenal ambao ni vinara mpaka sasa wa ligi kuu ya Uingereza wao watahitaji kushinda mchezo huu kwa kiwango kikubwa ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa huo msimu huu.

Chelsea wao pia mchezo utakua muhimu sana kwao kwani wakifanikiwa kushinda mchezo huu watakua na matumaini ya kucheza michuano ya ulaya mwakani,Ambapo kama watakosa ligi ya mabingwa basi watapata Uefa Europa league au Uefa Conference League.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye michuano mbalimbali barani ulaya na duniani kote. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Timu hizi zinakutana ambapo Arsenal atakua na kumbukumbu ya kusimamishwa na Chelsea wakiwa na fomu nzuri kabisa na kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Hivo mchezo wa leo ndio utaamua ni nani mbabe wa mwenzake katika msimu huu wa 2023/2024.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUJIUNGA NA GEITA GOLD...JINA LA SAIDO NTIBAZONKIZA LATAJWA TENA YANGA...KAZE ASHINDWA KUJIZUIA...