Home Habari za michezo FT: YANGA 2-1 SIMBA SC…..GUEDE, FREDY WAINGIA KWENYE REKODI YA DERBY….UBINGWA BADO...

FT: YANGA 2-1 SIMBA SC…..GUEDE, FREDY WAINGIA KWENYE REKODI YA DERBY….UBINGWA BADO 6 TU…

Habari za Michezo leo

Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya kuichapa kwa mara ya pili ndani ya Ligi Kuu Bara katika msimu mmoja kutokana na kushinda mabao 2-1, leo Jumamosi, huku ikibakisha kushinda mechi sita kati ya nane ili kutetea ubingwa wake.

Yanga imeibuka na ushindi huo kutokana na mabao ya Stephanie Aziz Ki dakika ya 20, akifunga kwa penalti, baada ya kufanyiwa faulo na Hussein Kazi, kisha Joseph Guede akafunga la pili dakika ya 38 kwa ufundi mkubwa akipokea pasi ya Khalid Aucho.

Simba ilipata bao lake dakika ya 74, likifungwa na Freddy Michael Koublan, aliyemalizia vizuri baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga ambao walishindwa kuhimili utulivu na nguvu za mshambuliaji huyo.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 58 baada ya mechi 21, huku Simba ikisalia nafasi ya tatu na pointi zake 46 kutokana na kucheza mechi 20.

Katika mechi nane ambazo Yanga imebakiwa nazo, ikishinda sita, itafikisha pointi 76 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, hivyo itatangaza tena ubingwa. Simba ikishinda mechi zake zote tisa zilizobaki, itafikisha 73.

DAKIKA 6 ZA INONGA, LOMALISA

Mwanzoni tu mwa kipindi cha kwanza, timu zote zililazimika kufanya mabadiliko ya lazima yakitofautiana kwa dakika sita pekee, wakianza Yanga ambao beki wake wa kushoto Lomalisa Mutambala alipata maumivu ya mguu dakika ya tano na kushindwa kuendelea na mchezo, akitolewa dakika ya sita, nafasi yake ikichukuliwa na Nickson Kibabage.

Dakika sita baadaye, Simba nao ikapata pigo baada ya beki wake wa kati, Henock Inonga kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia kupata maumivu dakika ya 10 na kutolewa dakika ya 12, nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Kazi.

AZIZ KI ANAZIDI KUKIMBIA

Bao hilo la Aziz Ki, linamfanya kuendelea kumkimbia kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei toto’ katika mbio za ufungaji akifikisha mabao 15 akimuacha mwenzake mwenye mabao 13.

Kwa upande wa Guede, amefikisha mabao matatu msimu huu ndani ya Ligi Kuu akiendelea kuamka, huku akifunga kwenye mechi mbili mfululizo baada ya kutoka kuifunga Singida Fountain Gate kwenye mchezo uliopita, wakati Freddy akifikisha mabao manne.

SOMA NA HII  KISA UTAMU ANAOUPATA YANGA...OKRAH KAAMUA KUJILIPUA NA HILI AISEE....NI 🔥 🔥 🔥..