Home Habari za michezo HIVI NDIVYO DIARRA NA JOB WALIVYOIPAISHA YANGA CAF…MSTAA WA SIMBA MHHH…

HIVI NDIVYO DIARRA NA JOB WALIVYOIPAISHA YANGA CAF…MSTAA WA SIMBA MHHH…

Habari za Yanga leo

Kipa Djigui Diarra na beki wake Dickson Job wameongoza kuwa vinara waliocheza muda mwingi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wakiwaachg mbali hata watani wao Sinmba.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) msimu huu Diarra ameichezea Yanga dakika 900 katika mechi l0 sawa Job kipa huyo akikosa mechi moja tu ya makundi ya kwanza dhidi ya CR Belouizdad ambao Yanga iliongozvwa golini na kipa wao namba mbili Metacha Mnata wakipoteza kwa mabao 3-0.

Nyuma ya ya Diarra na Job wamo Aziz KI na kiungo Maxi Nzengeli ambao wamecheza mechi 10 wakitumig dakika 839 kila mmoja.

Kwa upande wa Simba staa ambaye ametumia muda mwingi msimu huu kwenye ligi ya Mabingwa ni beki na nahodha msaidizi Mohamed Hussein “Tshabalala’ ambaye kwenye mechi 10 alizoichezea Simba ametumia dakika 810 Nyuma ya Tshabalala wapo Fabrice Ngoma ambaye amecheza dakika 746 katika mechi tisa, Chemalone Fondoh dakika 740 mechi tisa wakati kipa Ayoub Lakred, mabeki Shomari Kapombe na Henock Inonga wakiwa wamecheza dakika 720 katika mechi nane kila mmoja.

Wapo wachezaji waliocheza dakika chache katika michuano hiyo kwa upande wa Yanga ni Zawadi Mauya amecheza mechi tatu akiwa na jumla ya dakika 38, Agustine Okrah dakika 32 mechi mbili, Mahlatse Makudubela (Skudu) mechi mnbili dakika 20 na Farid Musa aliyecheza mechi mbili dakika 16.

Simba nako wale waliocheza muda mchache zaidi wamo beki Davida Kameta ‘Duchu’ aliyetumika dakika 24 pekee, Fredy Kouablan dakika 48 kipa Aishi Manula aliyecheza dakika 90 wakati winga Luis Miquisone akicheza mechi sita akitumia dakika 206.

SIMBA KUNDI JEPESI
Achana na dakika za mastaa hao kwenye mechi za makundi kundi B ndio lililoonekana kuwa jepesi zaidi ambapo ndio pekee halijaingiza timu yoyote kwenye nusu fainali.

Kundi B ambalo lilikuwa na timu za Simba, ASEC Mimosas, Jwaneng Galaxy na Wydad Athletic timu zao mbili zilizotinga robo fainali kinara ASEC na Simba zimejikuta zikiishia hapo robo tu.

Yanga ambao walikuwa kundi B pamoja na Al Ahly, Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana wamefichiwa aibu na Waarabu hgo ambao ndio mabingwa watetezi walioitumia Simba kutinga nusu fainali baada ya kuwachapa jumla ya mabao 3-0.

Kundi A lililokuwa na timu za vinara Mamelodi Sundowns na TP Mazembe iliyoshika nafasi ya pili zimetinga nusu fainali, Nouadhibou na Pyramids lilionekana kuwa timu zilizotoka kundi gumu.

Nayo Esperance de Tunis imelilindia heshima kundi C Ikitinga nusu fainali ikiitoa ASEC Mimosas baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi hilo lililoongozwa na Petro Altetico ambao waliishia robo fainali.

SOMA NA HII  ZIMEVUJAAA....YANGA KULAMBA BILION 1 FEI TOTO AKIJIUNGA SIMBA...