Home Habari za michezo KUELEKEA KARIAKOO DABI….BOSI YANGA AFUNGUKA SIRI HII…BAADA YA KUTUA DAR

KUELEKEA KARIAKOO DABI….BOSI YANGA AFUNGUKA SIRI HII…BAADA YA KUTUA DAR

Habari za Yanga leo

Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kutokea Mwanza katika pambano lao dhidi ya Singida Fountain Gate, Mjumbe wa Kamati wa Utendaji Klabu ya Yanga, Alex Ngai ameuzungumzia mchezo wao ujao dhidi ya watani zao Simba SC.

Yanga watavaana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Jumamosi ijayo, Aprili 20, katika Dimba la Mkapa huku Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga Simba mabao 5-1 karika duru ya kwanza.

“Tuna timu bora na tuna kikosi bora hatuna kitu kingine zaidi ya ubora tunahitaji kupata alama tatu tu idadi ya magoli hatujui lakini alama tatu lazima watuachie.

“Hakuna dabi nyepesi, dabi ya Simba na Yanga siku zote ni ngumu lakini tunaamini tutapata ushindi. Hakuna kitu kingine tunachojivunia zaidi ya kuwa na timu bora ili ushinde. Tunaamini katika kucheza mpira uwanjani, mazoezi na maandalizi mazuri,” amesema Ngai.

SOMA NA HII  FEI TOTO AANZA TAMBO AZAM FC...AWATAJA MABEKI HAWA ANAWAOGOPA...AMEFUNGUKA HAYA