Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA SAUZI….PACOME AMPA TABASAMU ZITO GAMONDI….ISHU NZIMA IKO HIVI…

KUELEKEA MECHI YA SAUZI….PACOME AMPA TABASAMU ZITO GAMONDI….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Yanga leo

UREJEO wa baadhi ya wachezaji wake muhimu akiwemo Pacome Zouzoua ambao walikuwa majeruhi, umempa jeuri kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye anaamini kuwa wanaweza kwenda Afrika Kusini na kufanya vizuri katika mchezo wa robo fainali ya pili, Ijumaa ijayo ya Aprili 5 dhidi ya Mamelodi Sundowns F.C.

Yanga ikiwa katika kiwango bora bila ya Pacome, Khalid Aucho na Kouassi Attohoula Yao, ilitoka suluhu juzi, Jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Hivyo wanahitaji ushindi au japo sare ya mabao yoyote katika mchezo wa marudiano ili kutinga hatua ya nusu fainali.

“Siwadai wachezaji wangu hakika wamecheza vyema na kufuata maelekezo, tumekutana na timu kubwa na bora ambayo ina uzoefu na hii michuano, ukiwa mwalimu na wachezaji wakawa wanacheza kwa kufuata maelekezo yako basi unafurahia na ndio furaha niliyoipata hata kama hatujapata ushindi,” alisema kocha huyo na kuongeza;

“Kwa sasa tunaenda ugenini tukiwa na matumaini ya wachezaji wengine ambao walikosekana kutokana na kuwa majeruhi kurejea na ukweli ni kwamba natamani tucheze fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.”

Katika mchezo huo, Gamondi ameonyesha kuwa yeye ni aina ya makocha ambao wanaweza kubadilika muda wowote kulingana na mazingira kiasi cha kumpa wakati mgumu kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena ambaye alikiri hilo.

Gamondi aliamua kuingia na mabeki wa tatu wa kati ambao ni Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Dickson Job ambaye alicheza kulia ambako Yao na Kibwana Shomary ni majeruhi, huku katika eneo la kati ambalo alizoeka kucheza Aucho alimtumia Jonas Mkude na mbele akaanza na washambuliaji wawili.

Yanga ilikuwa bora katika kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza kupitia maeneo yote ya uwanja huku pasi za kuchana ukuta za Stephane Aziz Ki na Mudathir Yahya zingeweza kuipa ushindi mzuri Yanga kama zingetumiwa vyema na Kennedy Musonda na Clement Mzize ambao walikimbia nyuma ya ukuta na kutazamana na kipa Ronwen Williams (31), lakini mastraika hao kila mmoja kwa wakati wake alianguka mbele ya mlindamlango huyo wa Mamelodi anayesifika kwa ubora wake, na hivyo kushindwa kupiga mashuti sahihi.

Akiongelea mchezo huo, Mokwena amesema, “Ilikuwa mechi ngumu, Yanga imeonyesha ubora wa aina yake lakini jambo zuri ni kwamba tunaenda nyumbani hivyo tutatakiwa kuwa bora zaidi ili kufanikisha mpango wetu.”

Mbali na Pacome mchezaji mwingine ambaye anaweza kurejea kwenye mchezo wa robo fainali ya pili ni Aucho ambaye inaelezwa alihitaji kuwa sehemu ya mchezo wa kwanza lakini Gamondi hakutaka kuharakisha urejeo wake ili kutomhatarisha. Kwa upande wa Yao bado inaendelea kuwa asilimia 50 kwa 50 kama ilivyokuwa mwanzo.

KOCHA AHLY AITAZAMA YANGA

Kocha wa Al Ahly, Marcel Koller naye alikuwa mmoja wa wafuatiliaji wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns.

Kupitia Insta Story yake, kocha huyo aliuliza swali hili! “Nawe umeitazama mechi hii!?”

Ikumbukwe hawezi kukutana na Yanga au Mamelodi kama watafuzu kwenye hatua ya nusu fainali ila kama atafuzu fainali atakutana na watu wanaopita njia hii.

SOMA NA HII  BEKI WYDAD CASABLANCA AWAOGOPA SIMBA...AVUNJA UKIMYA...ISHU NZIMA IKO HIVI