Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWATUNGUA SIMBA JANA….GAMONDI KAIBUKA NA HILI KWA YANGA….

PAMOJA NA KUWATUNGUA SIMBA JANA….GAMONDI KAIBUKA NA HILI KWA YANGA….

Habari za Yanga

LICHA ya kuchora ramani nzuri ya kutwaa taji la ubingwa kwa msimu mwingine, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameendelea kusisitiza kuwa wanahitaji kupambana na kujitoa katika michezo iliyosalia ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema anaimani wametoka kwenye michezo migumu lakini anaamini wanapoelekea ni zaidi walipotoka hasa katika michezo saba iliyosalia ya Ligi hiyo kuhakikisha wanavuna pointi muhimu katika kila mchezo iliyopo mbele yao.

Gamondi amesema hayo mara baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo wa Kariakoo Derby kwa kufanikiwa kuvuna pointi tatu zingine mbele ya watani wao wa jadi Simba kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2 -1, uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Amewapongeza kwa utendaji mzuri wa kundi lake la wachezaji kwa tabia ya kupigiania na kupambania timu dhidi ya kuwepo kwa mambo ya nje ya uwanja ambayo watu wengine wanajaribu kufanya Nje ya uwanja ikiwemo sehemu ya vyumba vya kubadilishia nguo.

“Mambo muhimu zaidi ni kucheza ndani ya uwanja bila shaka tumefanikiwa mipango yetu, Najivunia wachezaji wangu maana hata kwa nyakati ambazo hawachezi vizuri lakini wanapambana kupata matokeo mazuri,” amesema Kocha huyo.

Ameongeza kuwa haikuwa mechi rahisi anafuraha na kujivunia kiwango vya wachezaji wake katika kila mechi ikiwemo Derby kucheza kwa tahadhari na kuwaheshimu wapinzani wao na kufanikiwa kuvuna pointi tatu zingine.

Kuhusu ubingwa amesema licha ya kuwa na mwanga nzuri lakini bado hawajihakikishii kuwa wameshakuwa na uhakika kwa sababu bado wana michezo takribani sana iliyopo mbele yao na anaimani ni migumu kuliko ambayo wametoka kucheza.

“Hatuna uhakika kwa asilimia zote kwa sababu tuna mechi za ushindani tunacheza Jumamosi nyumbani halafu tunaenda kucheza ugenini, tunahitaji kupata pointi muhimu katika hizo mechi kufikia malengo yetu,” amesema Kocha huyo.

Naye Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema mechi ilikuwa nzuri na ngumu kipindi cha kwanza dakika 10, waliweza kutengeneza nafasi mbili, shida bado iko palepale.

“Bado tatizo letu halijapata majibu tumetengeneza nafasi lakini kuyageuza kuwa mabao ni ngumu, lakini pia tulilazimika kufanya mabadiliko ya lazima baada ya Henock Inonga kuumia na mchezaji aliyekuja kuchukuwa nafasi yake yake akasababisha penalti na kuwapinzani kupata bao la kwanza.

Kuhusu ubingwa ni ngumu sana lakini bado tunatakiwa kupambana kushinda matokeo katika mechi zilizosalia. Baada ya kuwa nyuma ya bao mbili tulilazimika kuongeza watu mbele ili kuweza kupata bao na kufanikiwa kufunga moja,” amesema Matola.

Kuhusu safu ya ulinzi amesema bado wamekuwa wakiruhusu bao katika kila mechi na kuendelea kufanyia kazi katika sehemu zote za mapungufu kujiandaa na michezo iliyosalia kutojiondoa katika ramani ya kupambana katika vita vya kuwania ubingwa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSHUSHIWA MASHINE YA KAZI...GAMONDI AANZA UPYAA YANGA...