Kipa wa kikosi cha Young African na timu ya Taifa ya Mali, Djigui Diarra ndiye mlinda mlango Wanza kufikisha clean sheets 12 kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu licha ya kukosekana kwenye michezo kadhaa hapo awali.
Diarra aliyekuwa amegongana na kipa wa Coastal Union, Ley Matampi wote walikuwa na clean sheets 10 kabla ya timu hizo kukutana Jumamosi na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wagosi wa Kaya.
Takwimu za Djigui Diarra katika ligi tangu ulipoanza msimu huuu
◉ 87 — Mechi
◉ 10 — Mabao aliyoruhusu
◉ 12 — Clean sheets
◉ 01 — Pre assist.
Itakumbukwa kuwa, Diarra anashikilia tuzo ya kipa Bora wa msimu wa Ligi kuu ya NBC akiwa amenyakuwa tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo tangu tu alipotua Jangwani.
Kabla ya Diarra, rekodi ya kuchukua golden gloves ilikuwa ikishikiliwa na Aishi Manula ambaye alinyakua tuzo hiyo kwa miaka mitano mfululizo, lakini kwa mwenendo wake sasa ni kama ameweka silaha chini na kumwachia ufalme huo Diarra.