Habari za Simba leo
Habari za michezo

MENEJA WA KIBU DENIS AFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA…AMEFUNGUKA HAYA A-Z

Marce Ben Komba May 9, 2024 8:30 pm

Meneja wa mchezaji wa Simba SC, Kibu Denis aitwaye Carlos Slyvester amesema kuwa sakata la mchezaji wake na Klabu hiyo lolote linaweza kutokea.
Kibu yupo kwenye mazungumzo na klabu yake hiyo kutaka kuongeza mkataba licha ya taarifa kusambaa kuwa amegoma akitaba aongezewe maslahi.

“Ni kweli nimepokea ofa kutoka Simba SC na Young Africans, ninaendelea kuzifanyia kazi, timu ambayo itafikia maslahi basi itafanikisha saini ya mteja wangu ingawa lolote linaweza kutokea.

“Kwa pande zote mbili Simba SC na Young Africans mazungumzo yapo na yanaendelea vizuri, pia sio ofa hizo tu, zipo nyingine kutoka nje ya Tanzania lakini hatuwezi kuweka wazi kwa sasa.

“Kwa timu zote mbili bado makubaliano hayajafikiwa mambo yakienda sawa moja kati ya timu hizo kila kitu kitawekwa wazi mtafahamu kwani mchezo wanaocheza wachezaji ni wa wazi,” amesema Carlos Slyvester.

TETESI:YANGA YAFUNGIWA USAJILI…ALLY KAMWE :- “TUNADAIWA MADENI NA WACHEZAJI FEI TOTO AWAKATAA MASHABIKI WA SOKA…”SISHINDANI NA MTU UWANJANI