Home Habari za michezo AHMED ALLY:- KWA SIMBA HII YA MGUNDA TUNAMFUNGA AL AHLY NNJE NDANI…

AHMED ALLY:- KWA SIMBA HII YA MGUNDA TUNAMFUNGA AL AHLY NNJE NDANI…

Habari za Simba leo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanatamani kurudiana na timu zote walizocheza nazo msimu huu zikawafunga.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Hii ni salam kwa yeyote anayekuja, Simba imeshika moto. Tunatamani wale wote ambao tumecheza nao kama kuna nafasi ya kurudiana nao muda huu, Simba SC tupo tayari. Simba hii kama tunapewa Al Ahly turudiane nao Ligi ya Mabingwa Afrika, anakufa nyumbani na ugenini, hilo wala halina mashaka.

“Hawezi kukukosa Chasambi, Karabaka au Balua, ngoma ikiwa ngumu atakufunga hata kocha. Mtazame Fredy alivyokuwa anawapeleka moto mabeki wa Azam FC. Simba sasa ipo sawa sawa, yeyote anayetaka aje,” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi, Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25, Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba Sc ni dhidi ya Kagera Sugar FC unaotarajiwa kuchezwa leo siku ya Jumapili ya Mei 12, 2024.

SOMA NA HII  JUMA MGUNDA...AKABIRIWA NA MTIHANI HUU MZITO SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z