Home Habari za michezo CHIRWA AVUNJA UKIMYA KUHUSU MASTAA WA BONGO…”TATIZO WANADHARAULIWA SANA…”

CHIRWA AVUNJA UKIMYA KUHUSU MASTAA WA BONGO…”TATIZO WANADHARAULIWA SANA…”

Habari za Michezo leo

Nyota wa klabu ya Kagera Sugar Obrey Chirwa anaamini kuwa nyota wazawa hawapewi heshima wanayostahili kutokana na ubora walionao ambao kwa wakati mwingine wanawazidi wageni wanaoimbwa kila siku.

“Nimekutana na makipa bora wengi nimekutana na Aishi Manula yule bora, nikakutana na Beno Kakolanya bora lakini Watanzania mnawadharau tatizo lenu, mnapenda vipya.”

“Watanzania wana uwezo mkubwa kushinda hata wageni ambao mnawaona kila siku mna wadharau.Mnaona safu ya mbele ya Yanga ile ni Watanzania ambao mnawaona wa kawaida lakini nchi nyingine ni bora wale.”

“Watanzania wengi ni hatari.Feisal, Muda ni Watanzania wanajua mpira.”

“Fei toto na Aziz Ki, Fei yupo juu wanamchukulia poa kwa sababu ni Mtanzania.”

SOMA NA HII  KUHUSU KUONDOKA AU KUBAKI YANGA...AZIZI KI AVUNJA UKIMYA....MSIMAMO WAKE MPYA HUU HAPA...