Home Habari za michezo HIO YANGA MPYA WEKA MBALI NA WATOTO AISEE…ENG HERSI KUSHUSHA VYUMA HIVI...

HIO YANGA MPYA WEKA MBALI NA WATOTO AISEE…ENG HERSI KUSHUSHA VYUMA HIVI VYA KAZI…

Habari za Yanga leo

WAKATI ikiwa na kibarua kigumu cha kusaka pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, klabu ya Yanga inahusishwa kutaka kuwasajili nyota, kiungo mshambuliaji, Agee Basiala kutoka klabu ya Maniema iliyopo nchini DR Congo na kipa wa Tanzania Prisons, Yoba Amos kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano.

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa timu hiyo upo kwenye mazungumzo na wachezaji hao, kwa upande wa Basiala nwenye uwezo wa kucheza namba nane na 10 pia anaweza kutokea pembeni alifanya mazungumzo na Rais wa Yanga, Hersi Said alipokuwa nchini DR Congo wiki iliyopita.

Kwa upande wa kipa Yanga, wapo katika mchakato wa kuhitaji huduma ya kipa huyo hudaiwa kwenda mitaa ya Jangwani kuchukuwa nafasi ya Metacha Mnata ambaye atapewa mkono wa kwa heri.

Taarifa za uhakika zilizoifikia Soka la Bongo kutoka ndani ya Yanga, kuwa Hersi amefanya mazungumzo na nyota huyo ili kuongeza nguvu ya timu pamoja na kiungo wa kati Yusuph Kagoma aliyekuwa Singida Fountain Gate FC.

“Mkakati mwingine wa mpango wa klabu unahusisha kipa wa Tanzania Prisons, Yona ni chaguo la kwanza kwa sasa, Yanga inalenga kupata huduma yake ili kuimarisha safu yao ya ulinzi na kuzidi kuimarika kama kikosi kikali katika soka la Tanzania,” amesema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa mazungumzo yakiendelea na mipango ya siku zijazo ikiendelea, Yanga imeendelea kujikita katika kudumisha hadhi yake ya kutawala soka la Tanzania, macho yakiwa yanalenga kuendelea kufanikiwa ndani ya timu ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mambo yanaenda vizuri na kil kitu kinasimamiwa ipasavyo na Rais timu, matumaini makubwa msimu ujao Wananchi watafurahi.

Katika hatua nyingine kikosi cha Yanga leo wanashuka dimbani katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Manungu Complex uliopo Tuliani Morogoro.

Kuelekea mchezo huo kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amesema maandalizi yaneenda vizuri, wanaiheshimu Mtibwa Sugar kwa sababu wako nyumbani na wapo nafasi ya chini na wanahitaji kupata matokeo chanya.

“Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu wapinzani wanaingia na presha kubwa ya kutaka kupata matokeo chanya, wachezaji wako tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kupambana kusaka alama tatu ,” amesema kocha huyo.

SOMA NA HII  YANGA YAMALIZANA NA MASHINE TANO... WAWILI WAFICHWA...SAKHO AWAGAWA MABOSI SIMBA..