Home Habari za michezo KIZUMBI ‘IN’ YANGA …KUPISHANA NA MUSONDA ANAYEENDA TP MAZEMBE…STAA MWINGINE HUYU HAPA..

KIZUMBI ‘IN’ YANGA …KUPISHANA NA MUSONDA ANAYEENDA TP MAZEMBE…STAA MWINGINE HUYU HAPA..

Tetesi za Usajili Yanga

KLABU ya Yanga imekamilisha usajili wa nyota wawili beki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, katika  timu za Saint Eloi Lupopo, Chadrack Boka na winga wa kulia wa TP Mazembe, Phillipe Kizumbi kwa ajili ya kujiimalisha na msimu ujao.

Imeelezwa kuwa Rais wa Yanga, Hersi Said amekabilisha dili hilo baada ya alipokwenda nchini DR Congo kufanya mazungumzo na viongozi wa Lupopo kwa kumsajili Boka anayekuja kuchukuwa nafasi ya Joyce Lomalisa mkataba wake unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zilizopatikana jana kuwa Hersi alifanya mazungumzo na Rais wa TP Mazembe, Moise Katumbi kwa ajili ya kutengeneza urafiki ikiwemo makubaliano ya kubadilisha mchezaji akiwemo Kizumbi kuja kucheza Yanga na Kennedy Musonda kwenda nchini Congo.

“Dili za wachezaji hao limekamilika kuwa Boka atakuja kuchukuwa nafasi ya Lomalisa ambaye atapewa mkono wa kwa kheri na kutoendelea na Yanga kwa msimu ujao, kuhusu Musonda amebakiza mkataba wa mwaka mmoja ataenda TP Mazembe akibadilisha na Kizumbi,” amesema mtoa habari huyo.

Katika hatua nyingine Mtendaji Mkuu wa klabu ya TP Mazembe, Frederick Kitengie yupo nchini na kukutana na Hersi pamoja na wajumbe wa Yanga kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ikiwemo suala la maendeleo ya klabu hiyo.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuhusu usajili unaendelea kufanywa kulingana na mapendekezo ya kocha Miguel Gamondi.

“Niwaambie mashabiki wa Yanga, kwa sasa wanatakiwa kufurahia ubingwa tukiwa na mechi tatu mkononi, suala la usajili mambo mazuri yanakuja na ukizingatia tumeingia ushirikiano na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo kwa kujifunza na kubadilisha ujuzi,” amesema Kamwe.

Naye Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick amesema wamefikiwa na ugeni mzito kutoka klabu ya TP Mazembe, Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, lengo ni kujifunza mambo mbalimbali kwenye mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji.

“Pia tutakuwa na makubaliano rasmi ya urafiki wa kushirikiana kati ya klabu yetu ya Yanga na TP Mazembe ili kuweza kubadilisha ujuzi wa mambo making ya kimpira yatakayowez kusaidia klabu yetu,” amesema Simon.

SOMA NA HII  MANARA: YANGA TUMEPOKEA OFA YA AL AHLY KUMTAKA NABI...KOCHA WA SIMBA KATUAIBISHA SANA...