- Habari za michezo
- Habari za Yanga
- Habari za Yanga Leo
- Michezo
- Michezo Bongo
- Michezo Soka la Bongo
- news
- Yanga SC
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.

Yanga walianza sherehe zao kuanzia mapema saa 4:00 asubuhi kwa mashabiki wao kunywa supu uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo kulianzia shamra shamra za kusherehekea Ubingwa wao.
Walipita Keko, Tazara, Buguruni, Karume. Mitaa ya Msimbazi na safari kuishia makao makuu ya klabu hiyo huku maelfu ya mashabiki wamejitokeza kwenye Paradi hiyo.
Walipowasili makao makuu ya klabu hapo Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe ametambulisha benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi na viongozi wa kamati ya utendaji inayoongozwa na Rais Hersi Said.
Nahodha Msaidizi wa Yanga, Dickson Job amesema anawashukuru wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa pamoja nao kwa msimu mzima na kuendelea kuwasapoti katika michezo iliyosalia.
“Kila mmoja anatambua kuwa Juni 2, mwaka huu kuna kibarua kigumu sana mbele yetu na tunaenda kupambana kuhakikisha tunafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na kuja kulitambulisha kwa mara nyingi hapa klabuni.

