Home Azam FC UNASHANGAA AZAM KUIPIKU SIMBA MSIMU HUU?….YANGA MJIAANDAE AISEE….BALAA LAO SIO POA…

UNASHANGAA AZAM KUIPIKU SIMBA MSIMU HUU?….YANGA MJIAANDAE AISEE….BALAA LAO SIO POA…

Habari za Michezo leo

Msimu wa Ligi Kuu Bara 2023/24, umekamilika hapo kesho jana kwa timu zote 16 kushuka kwenye madimba nane tofauti katika muda mmoja wa saa kumi alasiri.

Tayari bingwa Yanga alishapatikana mapema, na jana ligi ikamalizia kwa msisimko mkubwa sana kwa mbio za kuwania nafasi ya pili iliyotwaliwa na Azam FC na kuiacha Simba ikishika nafasi ya tatu ya kushiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Coastal Union ya Tanga iliyomaliza ya nne.

Kabla ya jana, ilikuwa ni Mtibwa pekee iliyoshuka daraja na hivyo kusubiriwa siku ya mwisho ya msimu kujua kwamba Geita Gold imeungana na wakata miwa hao kucheza Ligi ya Championship msimu ujao, huku JKT Tanzania iliyomaliza katika nafasi ya 13 na Tabora United (14) zitacheza mechi za play-offs kusaka timu ya kubaki na itakayofungwa itacheza na mshindi wa play-offs za Championship kujua hatima ya nani atacheza Ligi Kuu nani ataanguka.

Siku ya mwisho wa ligi jana pia ndio mshindi wa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha mfungaji bora alijulikana — Aziz Ki wa Yanga aliyefunga mabao 21 akifuatiwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam aliyefunga mabao 19.

Kukamilika kwa msimu huu ndiyo kuanza maandalizi kwa msimu ujao na tukizungumzia maandalizi, Azam FC ndiyo timu iliyoanza mapema zaidi.

Imekuwa ikitambulisha wachezaji wapya tangu mwezi Machi, wakianza na Yoro Diaby, mlinzi raia wa Mali kutoka klabu ya Stade Malien alikokuwa kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali.

Baadaye akatambulishwa Frank Tiesse kutoka timu hiyo hiyo, raia wa Ivory Coast aliyerithi kitambaa cha unahodha klabuni hapo kutoka kwa Djigui Diarra.

Wakati msimu ukielekea mwisho, Azam ikatambulisha wengine wawili kutoka Colombia; kiungo Ever Meza na mshambuliaji wa kati, Jhonier Blanco.

Na inasemekana hawajamaliza, bado kuna vyuma vinakuja. Haya yote ni maandalizi ya msimu ujao ikiashiria kwamba Azam FC kuna jambo wanalitafuta katila Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika ambako itashiriki.

Ukiangalia matokeo yao kwa misimu mitatu iliyopita, kuanzia 2021/22 pale ligi yetu ilipoanza kuwa na timu 16 kutoka 18 za msimu wa nyuma yake, utaona Azam FC inaimarika kidogo kidogo. 2023/24 P W D L GF GA GD PTS 29 20 6 3 61 21 +40 66 2022/23 P W D L GF GA GD PTS 30 18 5 7 55 29 +26 59 2021/22 P W D L GF GA GD PTS 30 14 7 9 41 28 +13 49

Baada ya kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya Geita Gold, Azam ikafikisha alama 69. Hili ni ongezeko la alama 10 kutoka msimu uliopita. Ukiangalia ‘hii trendi’ utaona Azam imekuwa ikiongeza alama 10 kila msimu.

2021/22 -Alama 49 2022/23 -Alama 59 2023/24 -Alama 69* Endapo msimu ujao itaongeza tena alama 10 maana yake itakuwa na alama 79. Hizo ndizo alama za mabingwa kila msimu tangu ligi iwe na timu 16.

2021/22 -Yanga alama 74 2022/23 -Yanga alama 78 2023/24 -Yanga alama 80 (NB: Yanga msimu huu ilitangaza ubingwa kwa alama 71 tu.) Ukiangalia rekodi za Azam FC katika misimu mitatu kwa kulingana na huu, utaona mabadiliko makubwa sana.

Msimu huu imefunga mabao mengi zaidi (63). Msimu huu imefungwa mabao machache zaidi (21). Msimu huu imevuna alama nyingi zaidi (69). Msimu huu imeshinda mechi nyingi zaidi (20). Msimu huu imepoteza mechi chache zaidi (3). Wasomi wanasema namba hazidanganyi, na kwa namba hizi za Azam FC, ni dhahiri kwamba kuna kitu ambacho inaweza kufanya msimu ujao. Ukichukua haya yote ukachanganya na aina ya wachezaji wanaosajiliwa, utanielewa.

1. Yoro Mamadou Diaby Ni zao la akademi ya Yeleen Olympique ya Mali, ambayo ni maarufu sana kwa kuzalisha vipaji.

Alizaliwa Februri 11, 2001 na sasa ana miaka 23. Amezichezea timu zote za taifa za vijana za Mali, kuanzia ile ya chini ya miaka 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.

Pia aliichezea timu ya taifa ya CHAN, akiwa nahodha msaidizi.

Katika mashindano hayo, Yoro alikuwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Angola, iliyoisha kwa sare ya 3-3.

Wakiwa nyuma 3-0 Mali walirudi kwa kishindo na kusawazisha, Yoro alifunga bao la kwanza dakika ya 72.

Akiwa na klabu yake ya Stade Malien, aliisaidia kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akifunga mabao katika mechi zote mbili za robo fainali, japo timu yake ilitolewa.

Mechi ya kwanza nyumbani iliisha kwa sare ya 1-1 na ugenini wakafungwa 2-1. Mabao yote ya timu yake akifunga yeye.

2. Frank Tiesse Ni raia wa Ivory Coast ambaye alicheza na Kipre Jr. kwenye klabu moja ya Sol FC (Stars Olympic FC) ya Ivory Coast.

Alizaliwa Desemba 17, 1997, akiwa na miaka 26 sasa. Yeye ndiye nahodha wa Stade Malien na alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho. Kwa mujibu wa mtandao ya FootMob, Tiesse alitengeneza nafasi 15 za mabao katika mechi 7 za Kombe la Shirikisho alizocheza.

Hizi ni nafasi nyingi zaidi katika mashindano ya msimu huu. Pia alifanikiwa kukokota mipira (dribles) mara nyingi zaidi na kuongoza kwenye mashindano ya msimu huu.

Kwa kifupi Tiesse ni zaidi ya Kipre Junior kwenye kutembea na mipira.

3. Ever Meza Kiungo wa mpira mwenye thamani ya juu. Jina lake kamili ni Ever William Meza Mercado. Alizaliwa Julai 21, 2000 huko Colombia.

Anacheza nafasi zote za kiungo na hata beki wa kati na pembeni. Ana uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Kombe la Shirikisho la CAF kwa hapa Afrika.

Alikuwa mchezaji wa timu ya Leonnes FC ambayo ilishuka daraja kwenye Ligi Kuu ya Colombia. Timu ikashuka lakini yeye hakushuka, akachukuliwa kwa mkopo kwenye timu ya Alianza FC. Akiwa na timu hii ndiyo akashiriki Copa Sudamericana.

4. Jhonier Blanco Mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza Colombia. Jamaa anajua kufunga, anajua kutafuta bao.

Jina lake kamili ni Jhonier Alfonso Blanco Yus. Alizaliwa Oktoba 18, 2000 huko Colombia na anakuja Tanzania akitokea klabu ya Aguilas.

Msimu uliopita, akiwa klabu ya Fortaleza, Blanco alikuwa mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza ya Colombia, akiwa na mabao 13.

SOMA NA HII  ACHANA NA BENCHIKHA KUSEPA ...FAILI LA 'MADUDU' YOTE SIMBA LIPO KWA MO DEWJI...