Home Habari za michezo YANGA BABA LAO UBINGWA WA FA…SIMBA WAFUATA NYUMA

YANGA BABA LAO UBINGWA WA FA…SIMBA WAFUATA NYUMA

yanga

UNAWEZA kusema kwamba Klabu ya Yanga ni Baba lao kwenye michuano hii ya Shirikisho, ambapo imechukua ubingwa mara 7, ikufuatiwa na Simba mara 4. Je miaka yote hiyo wengine walikuwa wapi?

Habarii za Yanga leo

Kuanzia mwaka 2003 michuano ya FA haikuwa ikichezwa, hadi pale Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF, walipopata udhamini na wa Azam Media na ndipo mwaka 2015 ilipoanza kuchezwa tena, huku Yanga wakiendeleza ubabe wao tangu waanze kulichukua mwaka 1967 lilikuwa linaitwa kombe la FAT ambapo Yanga iliifunga Liverpool ya ILALA Mabao 2-0

Yanga ilitwaa taji la wanza la ASFC, kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC, kabla ya Simba kufanya makubwa kwa kuifunga Mbao FC kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

MIKOA ILIYOPIGWA FAINALI.

2015-16- Benjamin Mkapa, Dar Es Salaam.
2016-17-Jamhuri, Dodoma
2017-18- Sheikh Amri Abeid, Ausha
2018-19-Ilulu Lindi.
2019-20-Nelson Mandela, Rukwa
2020-21- Lake Tanganyika, Kigoma
2021-22-Sheikh Amri Abeid- Arusha
2022-23-Mkwakwani Tanga
2023-24- New Aman, Zanzibar

MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO TANGU LIANZISHWE (FAT)

Yanga SC kachukua mara 7 kuanzia mwaka, 1967,1974,1999,2001,2015/16,, 2021/22, 2022/23

Simba kachukua ubingwa wa FA mara 4 (1995, 2016/17, 2019/20, 2020/21)

Azam FC wao wamechukua ubingwa huo mara moja tu mwaka 2018/18.

Timu zingine zilizowahi kuchukua ubingwa wa FA, Majimaji ya Songea 1985, Sigara FC, 1996, Tanzania Stars 1997, 1998, Mtibwa Sugar 2000, JKT Ruvu 2002, 2003-2015 Haikuchezwa, 2017/18

Je mwaka 2023/24 atachukua nani kati ya Azam FC vs Yanga SC?

SOMA NA HII  HIKI HAPA NDIO KILICHOWAPONZA YANGA DHIDI YA WAARABU