Home Habari za michezo SIMON MSUVA ATUA DAR USIKU…KISA TAIFA STARS…KIBU DENIS AKATAA KWENDA MAREKANI

SIMON MSUVA ATUA DAR USIKU…KISA TAIFA STARS…KIBU DENIS AKATAA KWENDA MAREKANI

taifa stars

Mshambuliaji wa Simba Kibu Denis ameonesha uzalendo mkubwa sana kwa kusitisha safari yake ya kwenda Marekani kwaajili ya mapumziko ya mwisho wa msimu, hii ni baada ya yeye kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

Jina jingine lilikuwa la Simon Msuva ambaye kwa sasa amekuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa Stars, awali alikataa kujiunga na wenzake kwenye kambi ta muda mfupi iliyowekwa huko Indonesia, na kudai kwamba akatiwe tiketi ya ndege hadi Zambia ili kuungana na wenzake.

Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Clifford Mario Ndimbo alitoa ufafanuzi juu ya taarifa za wachezaji hao alipotafutwa ili kuondoa sintofahamu iliyokuwa ikiendelea.

“Wachezaji ambao wameitwa ila hawaonekani, wapo kwenye majukumu mengine, watajiunga na timu itakaporejea nchini siku ya Jumanne (kesho) kutoka Indonesia kwaajili ya kusafiri kwenda Zambia” Clifford Ndimbo

Lakini kabla ya taarifa hizi kutoka TFF, ifahamike kwamba wachezaji kadhaa ambao waliitwa kwenye timu hiyo, kila mmoja kwa sababu zake walikataa kujiunga kwenye kambi ya muda mfupi huko Indonesia.

Mmoja wa wachezaji hao alisema kwamba awali hakuwa na taarifa kwamba amechaguliwa kujiunga na Taifa Stars.

“Ujue haya mambo yanachanganya sana, sikuwa na taarifa mapema, baada ya kikosi kutangazwa ndiyo nilijua nimechaguliwa timu ya Taifa, ila kabla ya hapo nilikuwa na ratiba zangu nyingine, hilo limenikwamisha” Maneno ya mchezaji huyo (jina linahifadhiwa)

Taifa Stars itacheza mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambai Juni 11 huko Zambia, mechi ya kundi E, Stars Inahitaji kupata ushindi ili kujiweka sehemu nzuri zaidi.

Mara ya mwisho timu hizi zilikutana kwenye fainali za mataifa ya Afriak, AFCON huko Ivory Coast hatua ya makundi ambapo timu hizo zilitoa sare ya 1-1, bao la Stars lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 11, huku kwa upande wa Zambia goli lilifungwa nna Patson Daka dakika ya 88.

SOMA NA HII  GAMONDI AMTAKA STRAIKA MWINGINE, MAMBO BADO SANA