news

KUHUSU KUJA AU KUTOKUJA KWA TP MAZEMBE..UONGOZI SIMBA WAFUNGUKA HAYA..WATAJA SABABU

admin September 10, 2021 3:00 pm


SIMBA imetaja sababu tatu za kuialika TP Mazembe kwenye kilele cha siku ya Simba Day, Septemba 19 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba itacheza na TP Mazembe mechi ya kimataifa ya kirafiki, timu ambayo ipo kambini ikikiwasha na waarabu nchini Morocco na sasa italazimika kupitiliza moja kwa moja Dar es Salaam.

Rais wa Simba Murtaza Mangungu amesema wameamua kucheza na Mazembe kwa kuwa ni miongoni mwa timu bora Afrika na ambayo msimu huu imefanya usajili wa aina yake.

Alisema mbali na kigezo hicho, pia walitaka kucheza na timu 10 bora za Afrika hivyo wanaamini itatoa upinzani wa kutosha kwa Simba kwani wako makini ndani na nje ya uwanja licha ya kejeli za mashabiki kwamba imechuja.

“Pia janga la corona limefanya mazingira ya timu kuingia na kutoka kwenye baadhi ya nchi kuwa magumu na kwenye baadhi ya nchi Ligi bado hazijamalizika,” alisema Mangungu huku akiwataka wanasimba kumiminika kwa wingi kwani Mazembe ni kipimo sahihi.

Alisema mbali na burudani ya soka, kwenye tamasha hilo mashabiki watapata zaidi ya burudani kwani Simba imesheheni na wachezaji wamepania kuonyesha uwezo mbele Mazembe ambao wamekuwa wagumu kufungika kwenye miezi ya hivikaribuni.

Mangungu alisema TP Mazembe watawasili nchini siku tatu kabla ya tamasha hilo ambalo wamepania msimu huu liwe na fleva za aina yake.

MANARA: WINGI WA MAKOMBE YA SIMBA NI WA MABONANZA KISA CAF KUZUIA WACHEZAJI YANGA…GSM AINGILIA KATI…AFANYA MAAMUZI MAGUMU..NABI ATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply