Home Habari za Simba Leo CHAMA AINGIA TAMAA…SIMBA WAWEKA NGUMU…MSHAHARA ANAOUTAKA

CHAMA AINGIA TAMAA…SIMBA WAWEKA NGUMU…MSHAHARA ANAOUTAKA

HABARI ZA SIMBA LEO-CHAMA

SAKATA LA CHAMA na Habari za Simba leo, Bado ngoma mbichi ambapo inaelezwa kwamba, kiungo huyo anataka kulipwa mshahara unaozidi wachezaji wote ikiwemo wa Winga Luis Miquissone   anayelipwa Tsh Milioni 44.

Clatous Chama bado hajasinya kandarasi nyingine ya kuendelea kukipiga Simba SC, baada ya mabosi wa Msimbazi kushindwa kumtekelezea mahitaji aliyowasilisha mezani ili asalie kikosini.

SUALA ZIMA LIKO  HIVI

Habari zinaeleza kwamba Utata umeibuka baada ya mabosi wa Simba kugomea kumuongezea ada ya usajili (sign on fee) ambayo, kiungo huyo alikuwa anaitaka ili asaini mkataba wa kuendelea kusalia katika timu hiyo.

Kwa Habari za Simba leo, Uongozi ni kama imeingia nyongo na Chama ambapo baadhi ya mabosi ndani ya klabu hiyo wanaona Mzambia huyo bado anahitajika, huku kundi jingine lenye nguvu likiona ni bora watengeneze timu mpya yenye ushindani bila mchezaji huyo.

Hatua ya pili ambayo Chama na Simba inabishana hadi sasa ni juu ya mshahara ambao anautaka, anataka alipwe sawa au zaidi ya Luis Miquissone.

Habari za Simba leo zinasema kuwa, mabosi wa Simba na Chama wameshindwa kuafikiana kwenye dau hilo la mshahara, kwani Mzambia huyo ametaka kulipwa Dola 20,000 (Sh 52 milioni) kwa mwezi.

Kwa sasa inadaiwa, Luis Miquissone ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza au kupata nafasi ya kutumika mara kwa mara kikosini, analipwa na Simba zaidi ya Dola 17,000 (Sh 44 milioni) kwa mwezi.

Mshahara ambao Chama ametaka zaidi ya kiwango hicho ili asaini mkataba mpya na mabosi wa Simba wanaona ni vigumu kumkubalia.

Hatua ya mwisho kwa Simba ni kama kundi linalotaka Chama aachwe linaelekea kushinda kwa vile wao ndio wanaotoa uamuzi makubwa ya bajeti ya klabu hiyo.

SOMA NA HII  AZIZ ANDABWILE AFICHUA SIRI YA USHINDI WA YANGA