Home Habari za Simba Leo KIMENUKA…VIONGOZI WA MATAWI SIMBA WAITANA…KIKAO KIZITO KUFANYIKA LEO

KIMENUKA…VIONGOZI WA MATAWI SIMBA WAITANA…KIKAO KIZITO KUFANYIKA LEO

HABARI A SIMBA LEO
SIKU chache tangu Uongozi wa Simba kutangaza mabadiliko makubwa, huku baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Lunyasi wakiachia ngazi, viongozi wa matawi wa klabu hiyo wameitana fasta ili kukutana kwa lengo la kujadili kilichotokea.
Simba ambayo ina misimu mitatu mfululizo ikicheza Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho bila kubeba ubingwa, imeelezwa ipo kwenye mipango ya kusafisha kila kitu kwa nia ya kuhakikisha msimu ujao inakuwa moto.
Tayari baadhi ya waliokuwa viongozi wakiachia ngazi kwa madai ya shinikizo la bilionea wa klabu hiyo, Mohamed ‘Mo’ Dewji aliyeingilia kati kuweka mambo sawa klabuni hapo.
Mjumbe wa Bodi ya wanachama wa Simba, Issa Masoud amesema viongozi wa matawi ya Simba wameitana na watakutana leo kuanzia saa 10:00 jioni kwenye ukumbi wa Gwambina (zamani TCC Chang’ombe) ili kuzungumzia mwenendo wa timu hiyo.
“Tunaenda kuyamwaga yote tumekaa sana kimya wanachama hawajui yanayoendelea wanasikia ya upande mmoja zaidi hivyo tunawaomba wanachama na viongozi wa matawi kujitokeza kwa wingi,” alisema Masoud.
Viongozi wa matawi wameibuka siku chache baada ya baadhi ya wajumbe walioteuliwa na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, MO Dewji ikielezwa ni moja ya mikakati ya kupanga upya safu ya uongozi.
Kwa lengo la kurejesha heshima ya Msimbazi iliyokuwa ikishikilia ubingwa wa Ligo Kuu kwa misimu minne mfululizo kabla ya watani wao, Yanga kupindua meza na kutawala kwa misimu mitatu mfululizo kwa sasa.
Wajumbe wa upande Mwekezaji ni Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Raphael Chageni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi ndio wamejiuzulu, huku wanne kati yao wakiachia ngazi akiwamo Shangazi aliyeweka wazi sababu za kufanya hivyo alipozungumza na wanahabari akiwa jijini Dodoma.
SOMA NA HII  MAYELE AWEKA REKODI HII YANGA...APEWA JEZI YA HESHIMA...ISHU NZIMA IKO HIVI