Home Habari za Simba Leo KANUNI ILIYOWAONDOA TRY AGAIN NA WENZAKE SIMBA…MO DEWJI HAJAVUNJA SHERIA

KANUNI ILIYOWAONDOA TRY AGAIN NA WENZAKE SIMBA…MO DEWJI HAJAVUNJA SHERIA

habari za simba leo

PAMOJA na habari zote kusambaa kuhusu kujiuzulu kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni uhalali wa uamuzi  huo kikatiba ya timu hiyo ukoje? Soka la Bongo tumechimbua kipengele kilichompa nguvu MO Dewji ya kuwataka viongozi hao.

Mohammed Dewji aliwateua mwenyewe wajumbe hao, uamuzi wa kuwaomba wajiuzulu ameuchukua ili kutokiuka katiba ya klabu hiyo ambayo inafafanua kuwa mjumbe wa bodi atakoma kutumikia nafasi yake ikiwa mambo manne yatatokea.

“Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi aliyechaguliwa na kuteuliwa kwa mujibu wa ibara ya 27 ya katiba hii atakoma kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi iwapo atatenda au kufanya mojawapo ya mambo yafuatayo. (a) Kujiuzulu kwa maandishi na kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa bodi ya wakurugenzi. (b) Kutohudhuria mikutano minne mfululizo ya kawaida ya bodi ya wakurugenzi. (c) Anashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo,” inafafanua ibara ya 29 ya katiba hiyo.

Katika kuhakikisha Simba inakuwa imara msimu ujao, Dewji anatajwa kufanya maamuzi kadhaa ambayo anaamini yanaweza kuirudisha makali yake na kuepuka kile kilichotokea hapo nyuma.

Miongoni mwa hayo ni kuwa mstari wa mbele ni kushiriki kwa ukaribu mchakato wa usajili wa nyota wapya ambao wataitumikia klabu hiyo ikiripotiwa kwamba hakuridhishwa na namna timu hiyo ilivyokuwa ikiendesha zoezi hilo kwa miaka ya hivi karibuni.

Na katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa umakini na ubora wa hali ya juu, Dewji ameamua kuwaongeza watu wanne wazoefu wa masuala ya usajili kusimamia zoezi hilo ambao ni Simba imeshawarudisha Crecensius Magori, Mulamu Nghambi, Kassim Dewji na Sued Mkwabi.

Ikumbukwe wakati Magori akiwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo ndio aliifanya iwe na kikosi tishio akisajili nyota kama Clatous Chama, Luis Miquissone, Meddie Kagere na Pascal Wawa.

Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally aliwahi kunukuliwa akithibitisha kuwa mchakato wa usajili ni zoezi litakalosimamiwa na Dewji mwenyewe.

“Fedha yote ya usajili ya msimu ujao atatoa Dewji, na mzigo ambao umetengwa kwa ajili ya usajili ni mkubwa. Niwaambie, Mo tunaye sana na tunatamba naye, usajili huu unaokuja utausimamia mwenyewe kwa asilimia mia moja.

“Kwa hiyo wanachama na mashabiki msiwe na wasiwasi, atasimama mwenyewe kwa miguu miwili kuhakikisha wachezaji bora na wa gharama wanatua kwenye klabu hii, mateso, manung’uniko, masononeko sasa basi,” alisema Ally.

Dewji pia anasimamia mwenyewe mchakato wa kocha mpya, ambapo inaelezwa kuwa ameshakutana na mmoja nchini Dubai alipo kwa sasa akitaka timu hiyo iende kwenye maandalizi ya msimu katikati ya mwezi ujao.

SOMA NA HII  ROBERTINHO APANGUA KIKOSI UGENINI