Home Habari za Simba Leo TATIZO LA SIMBA NI MO DEWJI…HATAKI WAWEKEZAJI WENGINE

TATIZO LA SIMBA NI MO DEWJI…HATAKI WAWEKEZAJI WENGINE

Habari za Simba leo, Mo dewji

WAKATI watu wengi wanajiuliza tatizo la Simba ni nini? Jibu ni jepesi sana, tatizo kubwa la Simba ni Mo Dewji Lengo kubwa la huyu bwana ni kutaka kuwa mmiliko wa Simba na mara kadhaa ameshajitangaza hivyo.

Habari ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa 49% hataki kabisa kuisikia, anatengeneza mazingira ya kuipiga ‘shot’ Simba hadi lengo lake la kuimiliki klabu litimie.

Ifike wakati MO Dewji akubali kuwa mwekezaji wa Simba au kama vipi akaanzishe timu au anunue timu ili atimize lengo lake la kuwa mmiliki wa klabu.

Anaposema kuna watu wanamkwamisha anamaanisha wanamkwamisha kuimiliki Simba sio kuwekeza. Kama ni kuwekeza mchakato ungekuwa umeshakamilika miaka mingi nyuma lakini yeye anataka kuwa mmiliki zaidi ya 51%

Hata uendeshaji wa timu ni wa kienyeji tangu mwaka 2018 huku yeye akiwa kama mmiliki na hujitambulisha hivyo kote duniani.

Hayo ni maoni ya Mchambuzi Shafii Dauda, kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram. na wala msimamo wa Soka la Bongo.

Hata hivyo kauli ya muwekezaji Mohamed Dewji, Mo kuwa yeye ni mmiliki wa Simba, aliitoa alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Global Publishers, pale ambapo aliulizwa ni Simba kwako ni faida, furaha au hasara?.

MO Dewji alijibu “Kuinunua Simba kwangu ilikuwa ni hasara kubwa, hela nilizowekeza Simba ningenunua ndege, tangu niwe mmiliki wa Simba sijawahi”

“Leo ni miaka 6 imepita tangu niwekeze Bilion 20 Simba, ukipiga mahesabu hadi sasa ni kama Bilioni 50 nimewekeza Simba, ningependa raha zaidi ya Simba ningenunua ndege, nimepata fursa nyingi za kuwekeza timu za nje lakini nimewekeza Simba” MO Dewji akifanya mahojiano na lobal Publishers.

“Ukinambia kwamba Simba ni biashara, hapana, Simba kwangu ni hasara, kuna wawekezaji wengi wamepita Simba na Yanga sitaki kuwataja, wengio wamefilisika, Simba nimepata hasara na sio faida”

Mchakato wa mabadiliko ya Simba yakikamilika kila kitu kitakuwa sawa, na kitajulikana kwa undani wake juu ya mfumo na muundo wa Uongozi ukoje. Lakini faida ya kuwa na muwekezaji mmoja zipo ni nyingi pia uwekezaji wa hisa kwa wau wengi ni mfumo mzuri zaidi kibiashara na uendeshaji, wanachama na mashabiki wa Simba mtachagua ninyi timu yenu iendeshwe kwa mfumo gani.

SOMA NA HII  NABI AMPA WOSIA HUU AZIZ KI...AMCHANA MAKAVU LIVE...AMEZUNGUMZA HAYA